Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 11:45 ALFAJIRI
UONGOZI wa Yanga SC, chini ya Mwenyekiti, Aljah Yussuf Manji leo unatimiza mwaka mmoja madarakani.
Kufuatia kujiuzulu kwa viongozi wakuu, Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga, Makamu wake Davis Mosha, Yanga ililazimika kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi hizo na Julai 14 Manji akachaguliwa kuwa Mwenyekiti na Clement Sanga Makamu wake.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kulikuwa kuna nafasi nne pia za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji za kujazwa na Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Aaron Nyanda walichaguliwa.
Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, zaidi ya kutwaa Kombe la Klabu Afrika Mashariki na Kati, Kagame, Ligi Kuu Bara na kuipeleka timu Uturuki kwa wiki mbili, bado uongozi wa Manji hauna cha kujivunia katika klabu hiyo.
Yanga bado hawana hata Uwanja wa mazoezi na hosteli ya klabu, makao makuu Jangwani ipo katika hali mbaya. Mwaka umekatika na hakuna dalili za klabu kuanza kujiendesha kibiashara zaidi ya kubaki kuwa tegemeo.
Uongozi mpya Yanga, umeshindwa japo kuvutia makamapuni mapya kuidhamini klabu zaidi ya TBL, ambayo iliingia wakati Mwenyekiti wa klabu akiwa Imani Madega mwaka 2008.
Wakati Mohamed Dewji anaifadhili Simba SC alizivutia pia na benki za NBC na kampuni ya Tanga Cement kuidhamini klabu hiyo.
Kwa ujumla Yanga SC ya sasa ambayo inategemea ufadhili wa TBL na fedha za mifukoni mwa watu kujiendesha, haipo katika mikono salama na wakati wowote matajiri hao wakisusa, klabu itaporomoka mno kwa hadhi na kiuchumi pia.

![]() |
Waliopewa dhamana; Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kulia akiwa na makamu wake, Clement Sanga kushoto siku kama ya leo mwaka jana Diamond Jubilee. |
Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja, zaidi ya kutwaa Kombe la Klabu Afrika Mashariki na Kati, Kagame, Ligi Kuu Bara na kuipeleka timu Uturuki kwa wiki mbili, bado uongozi wa Manji hauna cha kujivunia katika klabu hiyo.
Yanga bado hawana hata Uwanja wa mazoezi na hosteli ya klabu, makao makuu Jangwani ipo katika hali mbaya. Mwaka umekatika na hakuna dalili za klabu kuanza kujiendesha kibiashara zaidi ya kubaki kuwa tegemeo.
Uongozi mpya Yanga, umeshindwa japo kuvutia makamapuni mapya kuidhamini klabu zaidi ya TBL, ambayo iliingia wakati Mwenyekiti wa klabu akiwa Imani Madega mwaka 2008.
Wakati Mohamed Dewji anaifadhili Simba SC alizivutia pia na benki za NBC na kampuni ya Tanga Cement kuidhamini klabu hiyo.
![]() |
Wapiga kura; Wanachama wa Yanga wakiwa na karatasi za kura, tarehe kama ya leo mwaka jana |
![]() |
Kila mtu alikuwa ana imani nao; Wanachama mbalimbali wa Yanga SC waliwaunga mkono Manji, Bin Kleb, Sanga na Katabaro, leo vipi? |