IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 10:00 ALFAJIRI
LIVERPOOL imeanza vyema mechi zake za kujiandaa na msimu mpya, baada ya kuifumua 4-0 Preston North End.
Philippe Coutinho alifunga bao la kwanza dakika ya 15 kwa penalti baada ya kuangushwa na kiungo wa Preston na wa zamani wa Liverpool, John Welsh.
Bao hilo lilifungua biashara nzuri ya mabao mengine matatu, yaliyofungwa na Jordon Ibe, Raheem Sterling na Iago Aspas.
Kocha Brendan Rodgers ambaye bado anaumizwa kichwa na mshambuliaji Luis Suarez, alikuwa mwenye furaha kutokana na matokeo hayo, beki mpya Kolo Toure aliyesajiliwa kutoka Manchester United aking'ara na uzi Mwekundu.
Mpya: Aspas amefunga bao lake la kwanza Liverpool katika ushindi wa 4-0 mjini Lancashire
La kwanza: Philippe Coutinho wa Liverpool akishangilia na mwenzake Jordan Ibe baada ya kufunga bao la kwanza
Anafungua akaunti: Ibe amefunga bao lake la kwanza
Coutinho akichuana na Paul Huntington wa Preston North End
Sura mpya: Wachezaji wapya Kolo Toure (kushoto) na Kevin Davies wa Preston