IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 9:30 USIKU
KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes jana ameanza kazi vibaya baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji Singha All Stars XI mjini Bangkok.
Bao lililomfanya Moyes aweke kumbukumbu ya kuanza vibaya Man United lilifungwa dakika ya 50 na mchezaji anayevaa jezi namba 14 wa All-Stars, Teeratep Wonothai kwa shuti la mbali.
Mwanzo mbaya: David Moyes amefungwa katika mechi ya kwanza kazini
Tom Cleverley akimtoka Mario Djurovski
Danny Welbeck akikabiliana na Kim Yoo-Jin
Ben Amos akipangua mpira huku Rio Ferdinand akiwa tayari kumsaidia.
11 walioanza: Hiki ndicho kikosi cha David Moyes katika mechi yake ya kwanza Man United