• HABARI MPYA

    Monday, July 15, 2013

    MAN UNITED CHALI, THIAGO AMALIZANA NA BAYERN MUNICH NA ATASAINI MIAKA MINNE

    IMEWEKWA JULAI 15, 2013 SAA 6:59 USIKU
    KLABU ya Manchester United imeangushwa katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania, Thiago Alcantara baada ya mchezaji huyo kukubali kujiunga na Bayern Munich akitokea Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 22.
    Kiungo huyo atasaini Mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ulaya na atakwenda kufanyiwa vipimo vya afya siku zijazo.
    Dili hilo pia linahusisha makubaliano ya klabu hizo mbili kucheza mechi ya kirafiki wakati fulani katika miaka minne ijayo, wakati Thiago suala lake binafsi limepata mwafaka mzuri.
    Big move: Thiago Alcantara has joined former manager Pep Guardiola at Bayern Munich
    Uhamisho mkubwa: Thiago Alcantara anajiunga na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola Bayern Munich

    "Thiago Alcantara alikuwa kivutio kikuu kwa kocha wetu mpya, Pep Guardiola,"amesema Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge. "Tunayo furaha ya kufanikisha uhamisho mkubwa. Thiago ametoka tu kuchaguliwa mchezaji bora wa michuano ya vijana ya Mataifa ya Ulaya chini ya umri wa miaka 21. Ni mchezaji mzuri ambaye ataongeza nguvu Bayern,".
    Gone: Thiago was frustrated at the lack of opportunities at Barcelona
    Amekwenda: Thiago alikerwa na kutopewa nafasi ya kutosha Barcelona

    Kiwango cha Thiago kimefanya azitoe mate klabu kadhaa kubwa Ulaya, ikiwemo United, na Guardiola aliripotiwa akisema kiungo huyo ni mchezaji nambari moja anayemtaka majira haya ya joto.
    Aling;ara na kuiwezesha Hispania kutwaa Kombe la Ulaya la U21, akifunga Hat-trick katika fainali dhidi ya Italia.
    Winner: Thiago celebrates with the UEFA European Under 21 Championship trophy
    Mshindi: Thiago akisherehekea na taji la UEFA la U21

    Alizaliwa Italia na wazazi Wabrazil, kabla ya kujiunga na akademi ya Barcelona alikofundwa soka ya kitaalamu hadi mwaka 2008 alipoanza kucheza. 
    Guardiola alimpandisha Thiago timu ya kwanza misimu miwili iliyopita na alicheza mechi 45, lakini maumivu yalimpunguzia idadi ya mechi hadi 36 msimu uliopita chini ya kocha Tito Vilanova, Barcelona ikitwaa ubingwa wa Ligi ya Hispania. 
    Pamoja na kuchezesha timu vizuri, kuwa na uwezo wa kupiga chenga na kufumua mashuti ya mbali, hakuweza kuwa chaguo la kwanza katika safu ya kiungo ya Barcelona mbele ya akina Andres Iniesta, Xavi Hernandez na Cesc Fabregas. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN UNITED CHALI, THIAGO AMALIZANA NA BAYERN MUNICH NA ATASAINI MIAKA MINNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top