Na Princess Asia, IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 4:08 USIKU
SIMBA SC leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mechi za kujiandaa na msimu baada ya kuwachapa wenyeji Kahama United bao 1-0 kwenye Mansipaa ya Kahama, Shinyanga.
Shujaa wa Wekundu hao wa Msimbazi leo alikuwa mshambuliaji mpya Zahor Pazi, aliyesajiliwa kutoka JKT Ruvu, ambako alikuwa anacheza kwa mkopo akitokea Azam FC.
Hilo linakuwa bao la kwanza la mtoto huyo wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na Simba SC, Iddi Pazi ‘Father’ tangu ajiunge na Wekundu hao wa Msimbazi majira haya ya joto, ambalo alifunga kipindi cha pili.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Omar Salum/Haruna Shamte, Mussa Mudde, Rahim, William Lucian ‘Gallas’, Marcel Kaheza, Abdallah Seseme/Felix Cuipoi, Edward Christopher, Sino Augustino na Ramadhan Singano ‘Messi’/Zahor Pazi.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ amesema kwamba baada ya mchezo huo, timu itaelekea Musoma mkoani Mara kucheza mechi moja zaidi.
Amesema mjini Musoma watacheza na kombaini ya Musoma kwenye Uwanja wa Karume Jumatano, yaani Julai 17 na baada ya hapo timu itarejea Dar es Salaam.
URA ya Uganda inatarajiwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na Simba SC Julai 20, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
Simba, kabla ya kwenda Kahama ilikwenda Katavi ambako ilicheza mechi mbili na kushinda zote, 3-1 dhidi ya Rhino FC ya Tabora na 2-1 dhidi ya kombaini ya Katavi kwenye Uwanja wa wazi wa Katavi mkoani humo.
Simba SC, ambayo ilikuwa Katavi kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchezo wake wa kwanza, mabao yake yalifungwa na Edward Christopher mawili na moja Nahodha mpya, Nassor Masoud ‘Chollo’ na mchezo uliofuata mabao yalifungwa na Kun James mshambuliaji aliye katika majaribio kutoka Al Ahly Shandi ya Sudan Kusini na beki Mganda, Samuel Ssenkoom aliyesajiliwa kutoka URA.

![]() |
Amefungua akaunti ya mabao Msimbazi; Zahor Pazi (katikati) amefunga bao lake la kwanza Simba SC leo |