• HABARI MPYA

    Sunday, July 14, 2013

    ARSENAL NOMA BWANA WEE, YAPIGA MTU 7-0 MAN CITY NA MAN UNITED ZIKICHEZEA VICHAPO VYA 'MADOGO'

    IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 3:30 USIKU
    MSHAMBULIAJI Olivier Giroud amefanya kazi nzuri ya kumshawishi kocha Arsene Wenger kwamba hahitaji kusajili mshambuliaji mpya majira haya ya joto kwa kufungwa mabao mawili katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Indonesia XI kwenye Uwanja wa Gelora Bung Karno, katika mchezo wa kwanza wa Arsenal kwenye ziara ya kujiandaa na msimu.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye alikuwa mshambuliaji chaguo la kwanza wa kati wa The Gunners msimu uliopita, alifunga mabao mawili ndani ya dakika nne mjini Jakarta baada ya kuingia akitokea benchi na kumkumbusha Wenger kwamba yeye anaweza kazi.
    Arsene Wenger alianzisha kikosi cha nguvu katika mchezo huo wa kwanza wa kujiandaa na msimu, akiwapanga nyota kama Mikel Arteta, Per Mertesacker, Theo Walcott, Alex Oxlade-Chamberlain, Aaron Ramsey na Kieran Gibbs.
    Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Walcott dakika ya 19, Akpom dakika ya 54, Podolski dakika ya 83, Olsson dakika ya 85 na Eisfeld dakika ya 87.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski/Martinez dk68, Jenkinson/Sagna dk68, Miquel, Mertesacker/Koscielny dk46, Gibbs; Arteta/Zelalem dk46, Ramsey/Rosicky dk68, Oxlade-Chamberlain/Olsson dk46; Gnabry/Podolski dk68, Akpom/Giroud dk68, Walcott/Eisfeld dk46.
    Pick that one out: Olivier Giroud netted a superb second goal to make it four
    Mkwaju: Olivier Giroud akifunga bao tamu la pili, ambalo lilikuwa la nne
    That's entertainment: Giroud entertains the fans before the match
    Missed out: Jack Wilshere did not play because of flu
    Mitutu mikubwa: Olivier Giroud (kushoto) alianza kudansi alipotokea kwenye Luninga kubwa, wakati Jack Wilshere (kulia) hakucheza sababu ya kusumbuliwa na mafua
    Young Gunner: Gedion Zelalem (left) was given a run out in the second half by Arsene Wenger
    Mtutu mdogo: Gedion Zelalem (kushoto) alipewa nafasi na Arsene Wenger kipindi cha pili
    Hands up: Arsenal celebrate scoring during the friendly
    Mikono juu: Wachezaji wa Arsenal wakishangilia
    Arsenal Lukas Podolski (left)
    Super sub: Lukas Podolski (kushoto) aliingia na kufunga
    Giroud, left,
    Giroud, kushoto amefunga mawili
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL NOMA BWANA WEE, YAPIGA MTU 7-0 MAN CITY NA MAN UNITED ZIKICHEZEA VICHAPO VYA 'MADOGO' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top