IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 3:13 USIKU
ANGALAU David Moyes anaweza kujihisi ahueni ya kutopata kipigo kikubwa.
Kiasi cha saa 24 tangu kocha huyo mpya wa Manchester United aanze vibaya kazi kwa kipigo cha 1-0 kutoka kwa Singha All-Stars mjini Bangkok, jirani zake City na kocha wao mpya, Manuel Pellegrini walianza pia vibaya ziara yao ya kujiandaa na msimu nchini Afrika Kusini.
Kama Moyes, Pellegrini hajajisikia vibaya kwa sababu ndiyo kwanza nyota wake wanarejea kazini baada ya mapumziko na wachezaji kama David Silva, Sergio Aguero, Pablo Zabaleta na mchezaji mpya, Jesus Navas bado hawajajiunga na timu.
City imefungwa mabao 2-0 na wenyeji Supersport United ya Afrika Kusini leo, timu aliyowahi kuchezea kiungo Mtanzania, Suleiman Abdallah Matola aliyewika Simba SC enzi zake, ambaye kwa sasa amestaafu na kuwa kocha.
Mabao yaliyoizamisha City leo yalifungwa na Niang dakika ya 56 na Erasmus dakika ya 82.
Kikosi cha Supersport United kilikuwa; Williams/Fernandez dk32/Pule dk62, Moloi/Moeketsi dk43, Fransman, Diouf/Pietersen dk80, Mdledle, Gyimah, Doutie/Maluleke dk62, Maluleka, Nyondo/Niang dk32/Mulenga dk62, Mathebula/Erasmus dk62 na Chenene/Grobler dk62.
Manchester City: Hart/Pantilimon dk45, Richards/ Facey dk45, Kompany/Boyata dk45, Garcia/Nastasic dk45, Kolarov/Lescott dk45, Barry/Rodwell dk45, Fernandinho/Huws dk45, Razak/Sinclair dk45, Suarez/Y Toure dk45/Cole dk83, Nasri/Milne dk45 na Dzeko/Nimely dk45.
Kitu hicho: Matija Nastasic akishuhudia mpira wa kichwa wa Mame Niang ukitinga kwenye nyavu za City
Kifaa kipya: Mchezaji mpya wa Manchester City, Fernandinho hakuweza kuinusuru City kuchapwa
Kikosi cha nguvu: Vincent Kompany (kushoto) na Samir Nasri walianza Manchester City leo 
Heshima: Vincent Kompany (kushoto), Joe Hart (katikati) na Edin Dzeko (kulia) wakiwa wamepozi na jezi ya Nelson Mandela
Scott Sinclair alikuwepo