IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 10:29 JIONI
KLABU ya Manchester United iko tayari kusajili wachezaji bora duniani kama Cristiano Ronaldo au Gareth Bale, baada ya klabu kusema itampa sapoti David Moyes kama atataka kununua wachezaji wa bei mbaya.
Kocha mpya, Moyes hadi sasa amemsajili Guillermo Varela pekee kwa daua mbalo halikutajwa na litakuwa kiduchu tu.
Lakini, Mtendaji Mkuu wa klabu, Ed Woodward amesema mpunga upo wa kusajili wachezaji wenye vipaji na kwamba watakuwa kushindana na klabu yoyote hata kwa Pauni Milioni 60 au 70.
Mlengwa mkuu: Manchester United inaweza kuwa tayari kumsaini Gareth Bale majira haya ya joto
Heshima: Cristiano Ronaldo aligoma kushangilia alipoifunga United katika Ligi ya Mabingwa
Ataraudi nyumbani?: Ronaldo aliondoka United chini ya Sir Alex Ferguson kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 80 mwaka 2009 kuhamia
Vijana wa Barca: United pia imekuwa ikihusishwa na kutaka kuwasajili Thiago Alcantara (kushoto) na Cesc Fabregas (kulia)
Sapoti ipo: Kocha mpya, David Moyes (kushoto) ameahidiwa sapoti na Mtendaji Mkuu, Ed Woodward (kulia)