• HABARI MPYA

    Sunday, July 14, 2013

    VAN PERSIE ATUA SYDNEY KUIONGEZEA NGUVU MAN UNITED BAADA YA KUPIGWA JANA

    IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 10:18 JIONI
    KOCHA David Moyes ameongezewa nguvu katika timu yake, baada ya mshambuliaji Robin van Persie kuungana na kikosi cha Manchester United mjini Sydney kwa ajili ya mchezo wa pili wa ziara ya kujiandaa na msimu.
    Mholanzi huyo, ambaye aliwafungia mabao 30 Mashetani Wekundu katika msimu uliopita, alipewa muda maalum wa kuungana na tomu tofauti na wenzake, baada ya kumaliza kuitumikia timu yake ya taifa, Uholanzi na akakosa mechi ya kwanza ambayo United walifungwa 1-0 Singha All-Stars mjini Bangkok jana.
    Timu ya Uholanzi ilikwenda katika ziara bara la Asia, mwezi Juni, ambako walizufunga timu za China na Indonesia, huku van Persie akicheza mechi zote.
    Late arrival: Robin van Persie turns up at Manchester United's Sydney hotel
    Amechelewa: Robin van Persie ameungana na Manchester United hotelini mjini Sydney
    Itakuwa nafasi yake ya kukutana kwa mara ya kwanza na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes, aliyerithi mikoba Sir Alex Ferguson aliyestaadu baada ya msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VAN PERSIE ATUA SYDNEY KUIONGEZEA NGUVU MAN UNITED BAADA YA KUPIGWA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top