• HABARI MPYA

    Thursday, July 18, 2013

    MAN UNITED KWA HASIRA SASA YAMGEUKIA GARETH BALE NA PAUNI MILIONI 60 MKONONI

    IMEWEKWA JULAI 18, 2013 SAA 7:15 MCHANA
    KLABU ya Manchester United inaweza kugeuzia mawingo yake kwa Gareth Bale baada ya kumkosa mmoja wa wachezaji iliyokuwa inawataka sana. 
    Mabingwa hao wa Ligi Kuu wameshuhudia kiungo wa kimataifa wa Hispania chini ya umri wa miaka 21, Thiago Alcantara wa Barcelona akichagua kumfuata kocha wake wa zamani, Pep Guardiola klabu ya Bayern Munich. 
    Lakini United imedhamiria kumpa sapoti kocha wake mpya, David Moyes katika harakati zake za kuunda kikosi cha kutetea taji kwa kumnunulia winga wa Tottenham, Bale, ambaye alishinda tuzo tatu za Mchezaji Bora wa Mwaka msimu uliopita baada ya kufunga mabao 21 Spurs.
    Wanted man: Gareth Bale (left) has been linked with Real Madrid and now Manchester United
    Anayetakiwa: Gareth Bale (kushoto) amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid na sasa Manchester United
    Missing out: United had been targeting Thiago Alcantara (centre), who signed for Bayern Munich
    Ameota mbawa: United ilikuwa inamtaka Thiago Alcantara (katikati), ambaye amesaini Bayern Munich

    Beki kinda wa Uruguay, Guillermo Varela ni mchezaji pekee aliyesajiliwa na United majira haya ya joto, lakini klabu hiyo inaweza kuanza mpango wa kumsajili kwa Pauni Milioni 60 Bale mwezi huu, kwa mujibu wa Daily Mirror
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAN UNITED KWA HASIRA SASA YAMGEUKIA GARETH BALE NA PAUNI MILIONI 60 MKONONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top