IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 6:12 USIKU
KULIKUWA kuna mtu kwenye benchi la ufundi, lakini Manchester United imeendelea kuwa ile ile, ya ushindi baada ya kocha David Moyes kuiongoza timu hiyo kupata ushindi mnono wa mabnao 4-1 ugenini usiku huu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England.
Mfungaji bora wa msimu uliopita, Robin van Persie amefunga mabao mawili sawa na Danny Welbeck kuipa United pointi tatu muhimu.
Van Persie alifunga mabao yake katika dakika za 34 na 72 wakati Welbeck alifunga dakika ya 36 na 90 na bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa dakika ya 82 na Wilfried Bony.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley, Giggs/Rooney dk61, Welbeck na Van Persie/Anderson dk86.
Swansea: Vorm, Rangel, Flores, Williams, Davies, Britton/Bony dk46, Canas/Ki dk76, Shelvey, Dyer, Routledge/Hernandez dk46 na Michu.
Wekundu moto: Robin van Persie akiifungia Manchester United bao la tatu
Zamu ya Namba 10: Wayne Rooney amerejea kikosini Manchester United
Babu kubwa: Robin van Persie akifunga bao la kwanza
Imekaaje hii? Robin van Persie akishangilia na Patrice Evra baada ya kufunga
Ametulia tuli: David Moyes (katikati) akiwa Phil Neville wakiangalia United yao ikifanya maangamizi
Mawili: Danny Welbeck ameifungia mawili Manchester United
Wakati wa kusherehekea: Wachezaji wa United wakiungana na Welbeck kumpongeza
Mkali kuliko mwaka jana? Welbeck alifunga bao moja tu katika Ligi Kuu England msimu uliopita
Jose Canas akikabiliana na Welbeck
Wakati mzuri: Moyes akitoa maeekezo
Benchi: Rooney alianzia benchi
Wazza amerudi: Rooney akiingia kuchukua nafasi ya Giggs...lakini Van Persie alikuwa nyota