IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 12:20 ASUBUHI
NI bao moja tu lililopatikana, lakini mabao manne zaidi yangeweza kupatikana kama wachezaji wangetumia nafasi zao vizuri.
Salum Abdul Telela aliifungia Yanga SC dakika ya pili na dakika ya 11, John Raphael ‘Bocco’ alifanikiwa kumtoka Kevin Yondan na kumvuta kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ kutoka langoni, lakini akapiga nje.
Bocco alijaribu kupiga mpira akiwa amebanwa haswa na Yondan na kujikuta akimuumiza beki wa Yanga na kushindwa kuendelea na mchezo.
Dakika ya 15, Kipre Tchetche alimtoka Juma Abdul na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, bahati mbaya kwake, kipa Barthez akawahi kutoka na kuuchupia mpira miguuni mwake.
Barthez aliumia na kubaki anagaagaa chini pamoja na Kipre na Cannavaro.
Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyekuwa anafuatilia, akajaribu kuuchukua mpira ausukume wavuni, lakini ‘akajikanyaga kanyaga’ na kuishia kuusukuma mpira kidogo ukatoka nje. Barthez hakuweza kuendelea na mchezo akaingia Deo Munishi ‘Dida’.
Dakika ya 30, Tchetche alifanikiwa kuingia ndani ya 18 na kufumua shuti kali likagonga mwamba na kutoka nje, kufuatia pasi nzurI ya Bocco.
Baada ya koswakoswa hiyo, Yanga wakafanya shambulizi la kushitukiza na Aishi Manula alishindwa kuificha vizuri krosi ya Simon Msuva ikamponyoka na kwa bahati nzuri Erasto Nyoni akawahi kuiokoa isiende nyavuni.
Dakika ya 38, Kipre Tchetche tena aliingia kwenye 18, safari hii ikiwa upande wa kulia na akafumua shuti zuri, Dida akadaka.
Yanga nao wakapoteza nafasi mbili zaidi za wazi za kufunga kipindi cha pili- kwanza dakika ya 67 Telela aliunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima akiwa karibu kabisa na lango, kiasi kwamba yeye mwenyewe hakuamini akabaki kushika kichwa.
Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.
Bado, mbali ya nafasi hizo, mchezo ulikuwa wa mashambulizi ya pande zote mbili, ingawa ulisimama mara mbili kwa ajili ya makipa wa Yanga SC kutibiwa baada ya kugongana na wachezaji wa Azam, kwanza Barthez ambaye alitoka na baadaye Dida mwishoni kabisa kwa takriba dakika nne kila mmoja.
Ulikuwa mchezo mzuri ambao mtu unaweza kusikia fahari kuutazama- mchezo ambao unaweza kukubali ulikutanisha bingwa na mshindi wa pili ya Ligi Kuu ya nchi. Mchezo ambao unaweza kukiri ulikutanisha timu za kucheza michuano ya Afrika.
Kipa Aishi Manula alitukumbusha enzi za kipa hodari wa zamani nchini, Mwameja Mohamed kwa udakaji wake mzuri. Naam, huyo ndiye Tanzania One wa baadaye na bila shaka anaweza kufanya kile ambacho Mengi Matunda alishindwa, kipa mwingine aliyekuwa na umbo zuri na akatabiriwa kuwa Mwameja mwingine, lakini hakufika mbali.
Pale katikati ya Uwanja watu wanne walipachangamsha sana- Himid Mao na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kwa upande wa Azam na Athumani Iddi ‘Chuji’ na Salum Telela kwa upande wa Yanga SC.
Yanga SC walikuwa wanaonana vizuri na kwa staili yao ya sasa ya kuuchezea mpira, ilipendeza na kufurahisha mashabiki wake na Azam waliendelea na staili yao ya kushambulia moja kwa moja na haikuwa ajabu wao ndiyo waliopoteza nafasi nyingi zaidi ya wapinzani wao.
Na burudani nyingine ilikuwa upande walipokuwa wakikutana David Luhende na Khamis Mcha ‘Vialli’- walionyeshana kazi. Hapana shaka hiyo ndiyo soka ambayo wapenzi wa mchezo huo nchini wanapenda kuiona kila siku.
Hiyo ndiyo soka ambayo timu zetu zinatakiwa kucheza. Soka ya ushindani. Soka ya namna ile kama itabeba taswira ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hakika tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana. Hongera Yanga SC kwa kuanza msimu vizuri na kutwaa Ngao ya Jamii. Hongera Azam FC kwa soka safi iliyotengeneza mechi nzuri- vema mchezo ya jana ukabeba taswira halisi ya Ligi Kuu ya Bara. Jumapili njema.