• HABARI MPYA

    Sunday, August 18, 2013

    ROONEY SASA AAMUA KUBAKI MAN UNITED, IMEKULA KWAO CHELSEA

    IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 12:39 ASUBUHI
    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney hatimaye amekubaliana na ukweli kwamba hawezi kuruhusiwa kuondoka Manchester United kujiunga na Chelsea.
    Licha ya kuonyesha nia ya kutaka kwenda kuchezea timu ya Jose Mourinho, Rooney ameamua kutulia ili awe fiti kabisa, baada ya kukosa mechi za kujiandaa na msimu na United kutokana na kuwa majeruhi.
    Mshambuliaji huyo alicheza kwa mara ya kwanza chini ya kocha mpya, David Moyes katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu jana timu yake ikishinda 4-1 dhidi ya Swansea lakini, akatengeneza mabaso mawili baada ya kuingia akitokea benchi kipindi cha pili.
    Rooney hakwenda hata kushangilia na wachezaji wenzake mabao hayo.
    On the outside: Wayne Rooney (second left) appears not to celebrate Manchester United's third goal with team-mates
    Mbali kabisa: Wayne Rooney (wa pili kushoto) hakwenda kushangilia na wenzake bao la tatu 
    Peripheral figure: Rooney (eighth right) chats with referee Phil Dowd as United celbrate Danny Welbeck making it 4-1
    Hana habari: Rooney (wa nane kulia) akizungumza na refa Phil Dowd wakati wachezaji wenzake wa United wakishangilia na Danny Welbeck baada ya kufunga bao lililohitimisha ushindi wa 4-1
    Alishuhudia akiwa benchi wakati Robin van Persie akifunga bao la kwanza na Danny Welbeck akifunga la pili, lakini akaingia uwanjani dakika ya 62. 
    Rooney alikwenda kutengeneza bao la kwanza kipindi cha pili lililofungwa na Van Persie kabla ya kumtengenezea pia Welbeck nafasi ya kufunga bao la nne, lakini alijitenga kabisa wakati wenzake wanashangilia mabao hayo.
    Resignd to his fate: Rooney will remain a Manchester United player for this season
    Amesalimu amri: Rooney ataendelea kuwa mchezaji wa Manchester United msimu huu
    Under instruction: Rooney was a 61st minute substitute for Ryan Giggs, setting up two goals
    Chini ya maelekezo: Rooney aliingia uwanjani dakika ya 61 kuchukua nafasi ya kocha mchezaji, Ryan Giggs na kutengeneza mabao mawili
    "Wayne amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii, kwa sababu anataka kurudi kikosini,"chanzo kimesema.
    "Nafikiri amekiri hakuna namna klabu inaweza ingeweza kumuuza na ameamua kuendelea kufanya mazuri kama aliyofanya. Haitachukua muda mrefu kurudi kikosi cha kwanza,".
    Waiting game: Rooney sits alongside Wilfrid Zaha and Chris Smalling on the United bench
    Anaangalia mchezo: Rooney akiwa ameketi na Wilfrid Zaha na Chris Smalling katika benchi la United jana
    Baada ya mchezo wake huo wa kwanza wa Ligi Kuu England, David Moyes alisema: "Tumeweka mambo sawa. Wayne anajituma sana [mazoezini] na kwa mchezaji yoyote, unapovuka mstari wa kuingia uwanjani, unakwenda kucheza soka yako.’
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ROONEY SASA AAMUA KUBAKI MAN UNITED, IMEKULA KWAO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top