Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 12:45 ASUBUHI
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amempongeza na kumsifu beki wa Yanga SC, David Luhende kwa kucheza vizuri katika mchezo wa Ngao ya Jamii jana dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu yake ikishinda 1-0.
Tenga alimwagia sifa hizo Luhende baada ya mchezo huo, wakati akikabidhi zawadi za Medali kwa timu hizo.
Beki huyo wa kushoto wa Yanga SC, baada ya kuvikwa Medali yake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadik akaenda kumpa mkono Tenga kabla ya kuondoka.
Na beki wa kati wa zamani wa Yanga SC, Tenga akatumia fursa hiyo kufungua moyo kwake kwa kinda huyo; “Leo umecheza vizuri sana,”alisema Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Na beki huyo chipukizi wa Jangwani, akasema; “Asante sana,”.
Bila shaka Luhende sasa akiwa anaingia msimu wake pili Yanga SC tangu asajiliwe kutoka Kagera Sugar ya Bukoba, amefanikiwa kumpokonya namba Oscar Joshua upande wa kushoto.
Luhende aliitwa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kuziba nafasi ya Shomary Kapombe wa Simba SC aliyekwenda kwenye majaribio Ulaya na akacheza mechi yake yake ya kwanza dhidi ya Uganda, mjini Kampala, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Hata hivyo, siku hiyo Luhende alifanya ‘madudu’ baada ya kuunawa mpira peke yake akiwa ndani ya eneo la hatari na kusababisha penalti, iliyokwamishwa nyavuni na Brian Majwega na kuwafanya wenyeji waongoze 2-1 kabla ya kushinda 3-1 na kukata tiketi ya CHAN.

![]() |
Umetisha kijana; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadik akimvalisha Medali Luhende jana |
Na beki wa kati wa zamani wa Yanga SC, Tenga akatumia fursa hiyo kufungua moyo kwake kwa kinda huyo; “Leo umecheza vizuri sana,”alisema Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Na beki huyo chipukizi wa Jangwani, akasema; “Asante sana,”.
Bila shaka Luhende sasa akiwa anaingia msimu wake pili Yanga SC tangu asajiliwe kutoka Kagera Sugar ya Bukoba, amefanikiwa kumpokonya namba Oscar Joshua upande wa kushoto.
![]() |
Haya twende; David Luhende akimfunga tela Khamis Mcha 'Vialli' |