IMEWEKWA SEPTEMBA 6, 2013 SAA 10:34 JIONI
BEKI Eric Abidal ameishutumu Barcelona kwa jinsi walivyomuondoa katika klabu hiyo na kwamba hata hawakumlipa alipopona baada ya upasuaji wa ini.
Beki huyo Mfaransa ambaye anaichezea Monaco msimu huu baada ya kutemwa Barcelona amesema maoni kwamba hawezi tena kucheza soka ya ushindani yalitolewa na klabu hiyo.
Abidal ameliambia gazeti la L'Equipe: "Ikiwa Guardiola angebaki Barca kisha nami ningebaki. Ni mtu ambaye ananiheshimu na tumeendelea kuwasiliana. Ni kocha mzuri,".
Amelazimishwa kuondoka: Eric Abidal (juu) amesema angebaki Nou Camp
Pep sawa: Abidal hajamlaumu kocha wa zamani, Pep Guardiola ambaye bado anampa heshima ya kocha mzuri.
Mtoa uamuzi: Rais wa Barcelona, Sandro Rosell alichagua kumuuza beki huyo Mfaransa
Alikuwa Rais Sandro Rosell aliyetoa uamuzi wa kumuondoa Abidal ambaye sasa amarejea Ufaransa na beki huyo amesema: "Ilikuwa vigumu kuukubalia uamuzi wao. Lakini nilikuwa nina chaguo gani?
"Mambo ambayo Barca walizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari waliouitisha kutangaza kuondoka kwangu hayakuwa na maana sana. Haikuwa kuhusu fedha, kwa sababu wakati wa miezi ambayo nilikuwa ninaumwa, kla bu haikunilipa,".
Barcelona yenyewe imejiachia pigo katika safu yake ya ulinzi wa kati baada ya kukwama kumsajili Daniel Agger kutoka Liverpool.
Abidal ambaye kwa sasa anachezea katika moyo wa safu ya ulinzi wa timu zote, Ufaransa na Monaco alisema: "Katika umri wangu ni rahisi kucheza katikati nikiwa nimezungukwa na mabeki wa pembeni vijana wadogo. Lakini kitu cha msingi ni kwamba, kocha (Claudio Ranieri) anajua naweza kucheza nafasi zote,". Barcelona bado haijajibu tuhuma za mchezaji huyo.
Mkongwe wa Ufaransa: Eric Abidal (kulia) amecheza mechi zote tangu ahamie Ligue 1 katika klabu ya Monaco


.png)