IMEWEKWA SEPTEMBA 29, 2013 SAA 7:10 MCHANA
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Ibrahim Masoud 'Maestro' alimfuata Mrisho Ngassa jana karibu na chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake, kuzungumza naye. Maestro ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha Redio Clouds alikuwa akimlalamikia mchezaji huyo kutopokea simu zake. Ngassa aliisaidia Yanga kushinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
|