• HABARI MPYA

    Friday, October 18, 2013

    HOMA YA PAMBANO LA WATANI, PRESHA YA BEKI YA KUSHOTO SIMBA SC YAISHA

    Na Princess Asia, Kigamboni
    PRESHA ya beki ya kushoto kwa Simba SC kuelekea pambano dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yanga keshokutwa imekwisha, kufuatia kupona kikamilifu na kuwa fiti kwa beki Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ aliyesajiliwa msimu huu kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Issa amekosa mechi tatu zilizopita za Simba SC kutokana na kuwa majeruhi, lakini hivi unavyosoma habari hii, tayari beki huyo wa kupanda na kushuka haraka yuko kambini na wenzake Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam kwa siku ya tatu leo.
    Amefika Kigamboni; Issa Rashid 'Baba Ubaya' (nyuma) tayari yupo kambini Simba SC kujiandaa kumkabili Mrisho Ngassa

    Baba Ubaya amepona kwa asilimia 100 na yuko fiti kiasi cha kutosha kwa mchezo wa keshokutwa baada ya kupumzika kwa takriban wiki mbili na hapana shaka Simba SC itakuwa na mtu sahihi Jumapili upande wa kushoto.
    Presha ilikuwa kubwa kwa Simba SC juu ya beki ya kushoto kutokana na Baba Ubaya kuwa majeruhi, lakini hapana shaka kwa kupona kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 19, ameleta ahueni kwa kiasi kikubwa.
    Anaweza; Akiwa Mtibwa Sugar, Baba Ubaya aliwadhibiti mawinga wenye kasi kama Simon Msuva

    Yanga SC inatarajiwa kuwa mwiba zaidi upande wake wa kulia ambako atacheza Mrisho Khalfan Ngassa na maana yake huo utakuwa upande wa kushoto wa Simba SC.
    Hapana shaka Issa anaweza kumdhibiti Ngassa kwani alikuwa akifanya vizuri kazi hiyo alipokuwa Mtibwa Sugar kabla ya kutua Msimbazi.
    Kwa ujumla Simba SC inaendelea vyema na maandalizi yake kwa ajili ya mchezo dhidi ya watani na kiungo Henry Joseph ataendelea kuwa nje ya kambi hadi baada ya mechi hiyo, kufuatia kuwakera makocha wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni na Msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo.
    Hii haitajirudia Jumapili; Baba Ubaya nyuma ya Ngassa Simba na Mtibwa msimu uliopita
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HOMA YA PAMBANO LA WATANI, PRESHA YA BEKI YA KUSHOTO SIMBA SC YAISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top