Mshambuliaji wa Simba SC, Mrundi Amisi Tambwe amekuwa akishangilia kigumu bila tabasamu anapofunga mabao, kiasi kwamba mashabiki wakaanza kufikiri jamaa huwa hacheki kabisa, lakini jana kabla ya mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Chuoni ya Unguja, Uwanja wa Amaan, Zanzibar kamera ya BIN ZUBEIRY ilimnasa akitabasamu na mtu mzima kumbe ana mwanya 'bonge la handsome'. |
0 comments:
Post a Comment