MSHAMBULIAJI Leo Messi amewapashia misuli Manchester City kwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya soka ya Hispania, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Barcelona wa 6-0 dhidi ya Rayo Vallecano usiku huu.
Ushindi huo unaifanya Barca itimize pointi 57 baada ya kuchea mechi 23 La Liga na kupanda nafasi ya pili, nyuma ya Atletico Madrid yenye pointi 60, lakini imecheza mechi moja zaidi.
Real Madrid ina pointi 57 pia katika nafasi ya tatu kutokana na kuzidiwa wastani wa mabao na Barca.
Dole tupu: Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Rayo Vallecano Uwanja wa Nou Camp leo
Messi akimtungua kipa wa Rayo Vallecano, Ruban Martinez
Messi alifunga mabao yake dakika za 38 pasi ya Fabregas na dakika ya 68 pasi ya Sanchez,wakati mabao mengine yalifungwa na Adriano Correia dakika ya pili pasi ya Pedro, Sanchez dakika ya 53 pasi ya Messi, Pedro dakika ya 56 pasi ya FÃ bregas na Neymar dakika ya 89 pasi ya Iniesta.
Messi sasa ametimiza mabao 227 katika mechi 262 Hispania, akimpiku mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid, Di Stefano aliyefunga mabao 227 katika mechi 329.



.png)
0 comments:
Post a Comment