• HABARI MPYA

    Saturday, April 12, 2014

    MANNY PACQUIAO ULINGONI NA TIM BRADLEY LEO MGM GRAND...NI PAMBANO LA KUMALIZA UBISHI

    MABONDIA Tim Bradley na Manny Pacquiao jana wamepima uzito tayari kwa pambano lao la usiku wa leo ukumbi wa MGM Grand Garden mjini Las Vegas, Marekani ambalo litakuwa la marudiano.
    Bradley alimshinda Pacquiao katika pambano la awali, lakini mpinzani wake hakukubaliana na uamuzi wa majaji.
    "Nimeliangalia lile pambano mara kadhaa na hadi sasa sijaona na siwezi kufafanua kwa nini majaji walimpa ushindi Tim,"alisema.
    Mawe kwa kwenda mbele: Manny Pacquiao (kushoto) na Timothy Bradley wakiwa wamepozi kwa ajili ya picha baada ya kupima uzito janaPick me: Pacquiao is desperate for revenge after losing the first fight
    Pambano la kisasi: Pacquiao anataka kulipa kisasi katika pambano la Jumamosi usiku
    Flex: Pacquiao (left) will become only the second boxer to exceed $700 million in terms of PPV revenue
    Mbavu na misuli: Pacquiao (kushoto) atakuwa bondia wa pili kulipwa dola za Kimarekani 700 million in terms of PPV revenue

    Pacquiao atalipwa kiasi cha fedha kisichopungua dola za Kimarekani Milioni 20 katika pambano hilo la Jumamosi ukumbi wa MGM Grand Garden Arena litakalodumu kwa takriban dakika 36.
    Pacquiao pia atakuwa bondia wa pili kupata dola za Kimarekani Milioni 700 kwa malipo ya Televisheni katika historia ya mchezo huo, mwingine akiwa ni 
    Floyd Mayweather ambao wote wamempiku Oscar De La Hoya.
    Pambano lake la awali na Bradley alilipwa dola za Kimarekani Milioni 661, wakati Mayweather atapanda hadi dola Milioni 756 atakapopambana na Marcos Maidana mwezi ujao.
    Hao ndiyo mabondia waliovuna zaidi noti ulingoni tangu Pacquiao aweke rekodi ya kuwa bondia pekee asiye Mmarekani kuingia kwenye orodha ya tano bora ya malipo mazuri ya haki za Televisheni, ambayo Evander Holyfield na Mike Tyson wanashika nafasi ya nne na ya tano, nyuma ya De La Hoya.
    Pacquiao hajashinda kwa Knock-out (KO) tangu mwaka 2009, wakati left hook yake ilipowakalisha Ricky Hatton kwanza na baadaye Miguel Cotto.
    Bradley, alinufaika na uamuzi wa majaji dhidi ya Pacquiao na kisha akamdondosha Juan Manuel Marquez katika pambano lililofuata. Je, nani atakaa Jumamosi?
    Leaving the rest in the shade: Manny Pacquiao is a fusion of supreme fighter and politician
    Atanikoma: Manny Pacquiao pamoja na kuwa bondia mwenye mafanikio pia ni Mwanasiasa mkubwa na Mbunge nchini mwao
    The big one: Manny Pacquiao faces Timothy Bradley in Las Vegas on Saturday night
    Ukitaka kumuu nyani usimuangalia usoni: Manny Pacquiao kushoto na Timothy Bradley mjini Las Vegas jana wakati wa kupima uzito
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANNY PACQUIAO ULINGONI NA TIM BRADLEY LEO MGM GRAND...NI PAMBANO LA KUMALIZA UBISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top