Na Princess Asia, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Azam FC ya Dar es Salaam, Gaudence Exavery Mwaikimba amesema kwamba anamshukuru Mungu amekuwa na bahati nzuri ya kufunga mabao kwenye Uwanja wa Sokione mjini Mbeya.
Mwaikimba ameyasema hayo leo wakati timu yake inaondoka kwenda Mbeya, kumenyana na wenyeji Mbeya City Council (MCC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja huo.
Azam inataka pointi tatu katika mchezo huo itangaze ubingwa na Mwaikimba amesema; “Mbeya ni nyumbani, nimecheza sana pale Sokoine tangu nipo mdogo sana, Uwanja ule naujua vizuri na hata kwenye giza naweza kucheza, uzuri nina bahati ya kufunga kwenye Uwanja ule,”.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Tukuyu Stars na Prisons zote za Mbeya amesema kwamba anakubalika sana Mbeya na ana mashabiki wengi, ambao hao humuunga mkono anapokuwa amevaa jezi ya timu yoyote.
Azam FC inaongoza Ligi Kuu iliyofikia ukingoni kwa pointi zake 56 baada ya kucheza mara 24, ikiwafunga tela mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia na Mbeya City pointi 46 za mechi 24 katika mbio za ubingwa.
Iwapo, Azam itaifunga Mbeya City itajihakikishia ubingwa, kwani itafikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote baada ya mechi za mwisho Aprili 19.
Yanga SC ambayo kesho inacheza na JKT Oljoro mjini Arusha, itamaliza na mahasimu Simba SC Uwanja wa Taifa, wakati Azam itamaliza na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Hata hivyo, Yanga SC wana malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya mchezaji Mohamed Netto wa JKT Mgambo aliyecheza siku wanafungwa mabao 2-1 na timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Lakini kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, malalamiko hayo hayawezi kupangua matokeo iwapo madai ya Yanga yataonekana yana ukweli, bali zitatolewa adhabu tu kwa ama kwa timu au mchezaji.
MSHAMBULIAJI wa Azam FC ya Dar es Salaam, Gaudence Exavery Mwaikimba amesema kwamba anamshukuru Mungu amekuwa na bahati nzuri ya kufunga mabao kwenye Uwanja wa Sokione mjini Mbeya.
Mwaikimba ameyasema hayo leo wakati timu yake inaondoka kwenda Mbeya, kumenyana na wenyeji Mbeya City Council (MCC) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye Uwanja huo.
Azam inataka pointi tatu katika mchezo huo itangaze ubingwa na Mwaikimba amesema; “Mbeya ni nyumbani, nimecheza sana pale Sokoine tangu nipo mdogo sana, Uwanja ule naujua vizuri na hata kwenye giza naweza kucheza, uzuri nina bahati ya kufunga kwenye Uwanja ule,”.
![]() |
Mfalme wa Mbeya; Mshambuliaji wa Azam FC amesema kwamba ana bahati ya kufunga Uwanja wa Sokoine wakati kesho timu yake inamenyana na Mbeya City |
Azam FC inaongoza Ligi Kuu iliyofikia ukingoni kwa pointi zake 56 baada ya kucheza mara 24, ikiwafunga tela mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia na Mbeya City pointi 46 za mechi 24 katika mbio za ubingwa.
Iwapo, Azam itaifunga Mbeya City itajihakikishia ubingwa, kwani itafikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote baada ya mechi za mwisho Aprili 19.
Yanga SC ambayo kesho inacheza na JKT Oljoro mjini Arusha, itamaliza na mahasimu Simba SC Uwanja wa Taifa, wakati Azam itamaliza na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Hata hivyo, Yanga SC wana malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya mchezaji Mohamed Netto wa JKT Mgambo aliyecheza siku wanafungwa mabao 2-1 na timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Lakini kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, malalamiko hayo hayawezi kupangua matokeo iwapo madai ya Yanga yataonekana yana ukweli, bali zitatolewa adhabu tu kwa ama kwa timu au mchezaji.
0 comments:
Post a Comment