NYOTA aliyeng’ara katika Kombe la Dunia Brazil, James Rodriguez anaondoka kwenye michuano hiyo baada ya timu yake kulala 2-1 mbele ya wenyeji, Brazil, lakini akiwa amenyoosha mkono kwenye kiatu cha dhahabu.
Chipukizi huyo wa Monaco ya Ufaransa leo amefunga bao la sita katika mashindano hayo, akiendeleza utamaduni wake wa kufunga katika kila mechi tangu kuanza kwa michuano.
Rodriguez pamoja na kuwekewa ulinzi mkali na mabeki wa Brazil leo, lakini alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya 80.
WANAOWANIA KIATU CHA DHAHABU KOMBE LA DUNIA
6 - James Rodriguez (Colombia)
4 - Thomas Muller (Ujerumani), Lionel Messi (Argentina), Neymar (Brazil)
3 - Karim Benzema (Ufaransa), Arjen Robben (Uholanzi), Robin van Persie (Uholanzi), Enner Valencia (Ecuador), Xherdan Shaqiri (Switzerland)
(Maandishi yaliyolazwa nchi hizo zimetolewa Kombe la Dunia).
Sasa anaongoza kwa mabao, huku wanaomfuatia Thomas Muller wa Ujerumani, Lionel Messi wa Argentina na Neymar wa Brazil kila mmoja akiwa na mabao manne.
Karim Benzema wa Ufaransa, Arjen Robben, Robin van Persie wote wa Uholanzi, Enner Valencia wa Ecuador na Xherdan Shaqiri wa Uswisi, kila mmoja ana mabao matatu.
Nyota huyo anayezitoa udenda klabu kubwa za Ulaya hivi sasa, anarejea nyumbani huku akiwaombea dua mbaya wanaomfuatia kwa mabao wasifunge tena, ili ajifariji kwa kiatu cha dhabau cha kombe la Dunia baada ya kushindwa kutimiza ndoto za kutwaa taji hilo.
0 comments:
Post a Comment