GWIJI wa Manchester United, Ryan Giggs ametunukiwa Shahada ya heshima ya Udakatari wa Sayansi na Chuo Kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa katika michezo.
Giggs, am bate amestaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita na kuwa kocha, alitunukiwa heshima hiyo katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Victoria mjini Bolton mchana wa Ijumaa.
Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Wales, anaongezea Shahada hiyo katika OBE aliyopata kutoka kwa Malkia mwaka 2007 na MA aliyopokea kutoka Chuo Kikuu cha Salford mwaka uliofuata.
0 comments:
Post a Comment