Refa Mganda, Dennis Batte akitoka uwanjani huku akiona aibu baada ya 'kuiuma sana' Tanzania katika mchezo dhidi ya Msumbiji Uwanja wa Zimpeto jioni ya leo. Tanzania ilifungwa 2-1 na kutolewa katika hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco. Pamoja na kukataa bao zuri la kichwa la Said Mourad aliyeunganisha mpira wa adhabu wa Khamis Mcha 'Vialli', Batte aliwapigia filimbi za kuotea wachezaji wa Taifa Stars wakiwa hawajaotea. |
0 comments:
Post a Comment