BAO pekee la Radamel Falcao jioni hii limeipa Monaco ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal, katika Kombe la Emirates mjini London, lakini wenyeji wameondoka wakilia na refa Martin Atkinson kwa kuwanyima penalti ya wazi.
Upande wa pili wa sarafu, Arsenal watajilaumu wenyewe kwa kumruhusu mshambuliaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 53 kufunga kiulaini akiwa peke akiruka kuunganishia mpira nyavuni kwa kichwa.
Refa Atkinson alitoa mpira nje licha ya Chubo Akpom kuangushwa ndani ya eneo la penalti na kipa wa Monaco, Daniel Subasic, maamuzi ambayo yalizua mzozo kidogo kabla ya mchezo kuendelea.
0 comments:
Post a Comment