Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
BEKI wa kushoto wa Msumbiji, Daniel Almiro Lobo amesema kwamba mshambuliaji Thomas Ulimwengu anaweza kuwa nyota mkubwa katika Ligi ya Afrika Kusini, iwapo atahamia huko.
Lobo anayechezea Platinum Stars ya Afrika Kusini, alikuwa na jukumu la kumdhibiti Ulimwengu katika mechi zote mbili za kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza AFCON mwakani Morocco dhidi ya Tanzania, Dar es Salaam na Maputo.
Msumbiji iliitoa Tanzania kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya sare ya 2-2 Uwanja wa Taifa na ushindi wa 2-1 Uwanja wa Zimpeto, Maputo na sasa imetinga kwenye kundi lenye timu za Niger, Zambia na Cerpe Verde.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Maputo juzi wakati anarejea Afrika Kusini, Lobo alisema Ulimwengu ni mshambuliaji wa kiwango cha kidunia na anaweza kucheza popote.
“Thomas, namjua. Najua anachezea TP Mazembe na Samatta. Wote ni wachezaji wazuri. Ni kazi ngumu sana kumdhibiti Thomas, ana nguvu na kasi. Kama anakuja Afrika Kusini, atakuwa nyota mkubwa sana,”alisema Lobo.
Thomas alifanikiwa kutia krosi nyingi tu dhidi ya Lobo Dar es Salaam na Maputo, moja ikizaa bao la kwanza la Stars Dar es Salaam lililofungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Na Jumapili Uwanja wa Zimpeto, Ulimwengu alimtoroka vizuri Lobo, ambaye alimuangusha na kuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mcha, ukaunganishwa nyavuni kwa kichwa na beki Said Mourad, lakini refa Dennis Batte akakataa bao.
Stars ambayo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza AFCON mwaka 1980 enzi hizo bado ikiitwa Kombe la Mataifa Huru ya Afrika, sasa itasubiri mbio za kuwania fainali za michuano hiyo za mwaka 2017 nchini Libya.

![]() |
Almiro Lobo kulia akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry kushoto |
![]() |
Lobo akipiga hesabu za kumpokonya mpira Thomas Ulimwengu kushoto Uwanja wa Zimpeto |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Maputo juzi wakati anarejea Afrika Kusini, Lobo alisema Ulimwengu ni mshambuliaji wa kiwango cha kidunia na anaweza kucheza popote.
“Thomas, namjua. Najua anachezea TP Mazembe na Samatta. Wote ni wachezaji wazuri. Ni kazi ngumu sana kumdhibiti Thomas, ana nguvu na kasi. Kama anakuja Afrika Kusini, atakuwa nyota mkubwa sana,”alisema Lobo.
Thomas alifanikiwa kutia krosi nyingi tu dhidi ya Lobo Dar es Salaam na Maputo, moja ikizaa bao la kwanza la Stars Dar es Salaam lililofungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Na Jumapili Uwanja wa Zimpeto, Ulimwengu alimtoroka vizuri Lobo, ambaye alimuangusha na kuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mcha, ukaunganishwa nyavuni kwa kichwa na beki Said Mourad, lakini refa Dennis Batte akakataa bao.
Stars ambayo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza AFCON mwaka 1980 enzi hizo bado ikiitwa Kombe la Mataifa Huru ya Afrika, sasa itasubiri mbio za kuwania fainali za michuano hiyo za mwaka 2017 nchini Libya.
0 comments:
Post a Comment