TANZANIA ilihitimisha wiki vibaya, baada ya timu zake mbili za sika za taifa, ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys na ya wakubwa, Taifa Stars kutolewa katika michuano ya Afrika.
Serengeti Boys ilianza kufungwa mabao 4-0 na Afrika Kusini mjini Soweto baada ya sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya Taifa Stars kufungwa 2-1 na Msumbiji mjini Maputo baada ya sare ya 2-2 nyumbani pia.
Mchezo wa marudiano baina ya Serengeti na Amajimbos Watanzania hawakuuona kupitia Talevisheni, lakini kuna malalamiko, wenyeji walibebwa na marefa.
Mchezo dhidi ya Msumbiji Maputo, Watanzania wengi walifanikiwa kuuona kupitia Televisheni na wakashuhudia marefa wa Uganda, wakiongozwa na Dennis Batte wakiwapendelea waziwazi Msumbiji Uwanja wa Zimpeto.
Taifa Stars imetolewa katika hatua ya mwisho ya mchujo ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani kwa jumla ya mabao 4-3, baada ya awali kulazimishwa sare ya 2-2 Dar es Salaam na Mambas inaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia kupigania tiketi ya Morocco.
Hadi mapumziko, tayari Msumbiji walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Josimar Machaisse dakika ya 45 aliyeunganisha krosi kutoka upande wa kulia.
Stars ilicheza kwa kujihami tangu mwanzo na kujibebesha mzigo wa kudhibiti mashambulizi mfululizo ya Mambas, huku yenyewe ikishambulia kwa kushitukiza.
Pamoja na mfumo huo, mashambulizi machache ya Stars yalikuwa yenye uhai na kama si refa Dennis Batte kuwabeba wenyeji, Tanzania ingemaliza na bao kama si mabao dakika 45 za kwanza.
Batte alikataa bao zuri la kichwa la beki Said Mourad aliyeunganisha mpira wa adhabu wa Khamis Mcha ‘Vialli’ baada ya Thomas Ulimwengu kuangushwa dakika ya 17.
Mshika kibendera nambari moja alimnyooshea kibendera cha kuotea mshambuliaji John Bocco akiwa anakwenda kufunga, wakati alikuwa hajaotea dakika ya 44.
Pamopja na yote, mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Ally Samatta aliifungia Stars bao la kusawazisha dakika ya 75 baada ya kumkokota beki wa Mambas hadi karibu na lango la Msumbiji kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa.
Elias Pelembe aliiandikia Msumbiji bao la pili dakika ya 81 kwa shuti la mpira wa adhabu lililotinga nyavuni moja kwa moja, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari na Kevin Yondan.
Baada ya Mganda huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo, wachezaji wa Stars walimfuata kumlalamikia huku wakilia kwa kuwanyonga wazi wazi.
Stars ambayo mara ya kwanza na ya mwisho ilicheza AFCON mwaka 1980 enzi hizo bado ikiitwa Kombe la Mataifa Huru ya Afrika, sasa itasubiri mbio za kuwania fainali za michuano hiyo za mwaka 2017 nchini Libya.
Wachezaji wa Stars waliumizwa mno na matokeo hayo, haswa refa Batte na wenzake na wakiwa katika chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Zimpeto, wakajutia namna Mambas ilivyochezeshwa kwa haki Dar es Salaam.
Wakawa wanawastaajabu viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushindwa kutengeneza mazingira ya kubebwa na marefa kwenye mechi za nyumbani.
Huo ni mtazamo wa Watanzania wengine pia, kwamba TFF ni wazembe kwa kushindwa kutengeneza mazingira ya kubebwa na marefa nyumbani.
Hii maana yake, watu wanataka na TFF na hiyo ijiingize kwenye mchezo wa kurubuni marefa wazibebe timu za taifa nyumbani. Utawarubuni vipi bila kuwahonga fedha, jambo ambalo FIFA wanaita upangaji wa matokeo na adhabu yake ni kubwa na mbaya sana? Nini suluhisho la matatizo ya timu yetu ya taifa pamoja na changamoto zote hizi? Tukijaaliwa Jumapili tutaanzia hapa. Alamsiki.

0 comments:
Post a Comment