• HABARI MPYA

    Sunday, August 03, 2014

    LIVERPOOL YAWAFUMUA AC MILAN 2-0...NI WAO NA MAN UNITED KESHO MIAMI

    KLABU ya Liverpool itakwenda Miami kupambana na wapinzani Manchester United Jumatatu kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya AC Milan mjini Charlotte.
    Mabao ya Joe Allen na Suso yameifanya timu ya Brendan Rodgers ishinde mechi ya tatu katika Kombe la Kimataifa nchini Marekani.
    Liverpool tayari ilikuwa imejihakikishia kuongoza kundi lake kufuatia kipigo cha Manchester City kwa penalti 5-4 kutoka kwa Olympiacos baada ya sare ta 2-2.

    Mwanzo mzuri: Joe Allen akipongezwa na Rickie Lambert baada ya kuifungia bao la kwanza Liverpool dhidi ya AC Milan
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL YAWAFUMUA AC MILAN 2-0...NI WAO NA MAN UNITED KESHO MIAMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top