Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MAKIPA Mwameja Mohamed na Manyika Peter, wote wameonyesha wako vizuri kueleka mchezo wa kesho wa magwiji wa Tanzania, dhidi ya Real Madrid Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mazoezi ya jana, makipa hao pekee katika kikosi hicho walionyesha umahiri wa uokoaji michomo ya aina tofauti- ingawa si kwa kiwango cha enzi zao wakitamba katika soka ya Tanzania.
Krosi, kona na mashuti vyote walicheza tena kwa mbwembwe- kuashiria kwamba wako tayari kuzuia michomo ya akina Luis Figo kesho Taifa.
Mjadala uliopo sasa, nani ataanza kati yao kesho- na hilo ni jukumu la makocha Charles Boniface Mkwasa na Wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuamua.
Mwameja alimtangulia kipa mwenzake huyo uwanjani, akianza kutamba miaka ya 1980 hadi mwaka 2002 alipotungika daluga rasmi akiwa na Simba SC.
Manyika aliibuka mwishoni mwa miaka ya 1990 na akacheza hadi mwaka 2005 alipostaafu rasmi akiwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Enzi zao, wote walisifika kwa uchezaji wa penalti, Manyika akiwika Yanga SC na Mwameja Simba SC na kwa wakati tofauti, wote waliitwa Tanzania One wakiidakia Taifa Stars.
Mbali na Mwameja na Manyika, kikosi hicho pia kina mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu,
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo,
Viungo Athumani China, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda.

![]() |
Ataanza, au atasubiri? Mwameja Mohamed akipanga mabeki baada ya kuokoa mazoezini jana |
![]() |
Ujuzi hauzeeki; Mwameja Mohamed akiwa amedaka shuti la chini jana Taifa |
Mjadala uliopo sasa, nani ataanza kati yao kesho- na hilo ni jukumu la makocha Charles Boniface Mkwasa na Wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kuamua.
Mwameja alimtangulia kipa mwenzake huyo uwanjani, akianza kutamba miaka ya 1980 hadi mwaka 2002 alipotungika daluga rasmi akiwa na Simba SC.
Manyika aliibuka mwishoni mwa miaka ya 1990 na akacheza hadi mwaka 2005 alipostaafu rasmi akiwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Enzi zao, wote walisifika kwa uchezaji wa penalti, Manyika akiwika Yanga SC na Mwameja Simba SC na kwa wakati tofauti, wote waliitwa Tanzania One wakiidakia Taifa Stars.
Mbali na Mwameja na Manyika, kikosi hicho pia kina mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu,
![]() |
Manyika Peter akiwa amedaka shuti jana mazoezini |
![]() |
Manyika akiwa amedaka jana mazoeizni |
![]() |
Mwameja baada ya kupangua shuti jana mazoezini |
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo,
Viungo Athumani China, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda.
![]() |
Manyika kulia akimuangalia Mwameja anavyodaka mazoezini jana Taifa |
0 comments:
Post a Comment