• HABARI MPYA

    Saturday, August 02, 2014

    WENGER ASEMA CAMPBELL YUPO KWENYE MIPANGO YAKE YA MSIMU UJAO

    KOCHA wa Arsene Wenger amepuuza taarifa za kwamba atamtema Joel Campbell aondoke Arsenal msimu huu, akisema kwamba mshambuliaji huyo kinda yupo kwenye mipango yake ya msimu ujao.
    Nyota huyo wa Costa Rica mwenye umri wa miaka 22, aliwapagawisha mashabiki wakati wa Kombe la Dunia nchini Brazil, lakini akawa anahusishwa na kutolewa kwa mkopo kuelekea msimu ujao. 
    Wenger amesema atabaki na atacheza michuano ya Kombe la Emirates inayoanza wiki ijayo.

    Kifaa: Joel Campbell ataichezea Arsenal msimu huu kwa mujibu wa Arsene Wenger

    Yuko vizuri: Wenger akizungumza na Waandishi wa Habari jana kuhusu Kombe la Emirates

    "Ndiyo, yeye (Campbell) ni sehemu ya mipango yangu. Anaweza kucheza leo dhidi ya Benfica,"Wenger aliwaambia Waandishi wa Habari katika mkutano jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER ASEMA CAMPBELL YUPO KWENYE MIPANGO YAKE YA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top