KLABU ya Real Sociedad ya Hispania imemtangaza David Moyes kuwa kocha wake mpya, licha ya Mscotland huyo kusema ni 'maajabu ya mwaka' klabu hiyo kumpa Mkataba wa miezi 18.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 anafikiri majukumu aliyochukua na mazito mho katika timu hiyo ambayo haifanyi vizuri kwa sasa katika La Liga, wakati anahitaji kurejesha heshima yake baada ya kufukuzwa Manchester United Aprili mwaka huu.
Bahati mbaya, Phil Neville alikataa kuungana naye huko kama Kocha Msaidizi na sasa anatafuta mtu mwingine wa kufanya naye kazi Hispania. Bado haijulikani sasa Moyes atamchukua nani katika benchi lake la Ufundi.
0 comments:
Post a Comment