• HABARI MPYA

    Thursday, November 13, 2014

    IBRAHIMOVIC APAMBANISHWA NA VAN PERSIE NA DIEGO COSTA TUZO YA BAO BORA LA MWAKA

    MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ameingia kutetea tuzo yake ya Bao Bora la Mwaka, baada ya kutajwa katika orodha ya wanaowania tuzo ya Puskas 2014.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ni miongoni mwa wachezaji 10 walioingia kwenye orodha fupi iliyoandaliwa na FIFA, fbaada ya bao lake alilofunga dhidi ya Bastia katika Ligue 1 akiichezea klabu yake, Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
    Msweden huyo alishinda tuzo hiyo msimu uliopita kwa bao la umbali wa mita 30 alilofunga dhidi ya England katika ushindi wa 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki.
    2013 Puskas Award winner Zlatan Ibrahimovic has been nominated for this year's prize - which is given to the best goal scored
    Mshindi wa Puskas 2013, Zlatan Ibrahimovic ameingia tena kuwania tuzo hiyo

    Ibrahimovic anachuana na wakali kama Diego Costa na Robin van Persie kwenye orodha hiyo ya wachezaji 10 ya FIFA ambayo inatokana na maelfu ya mabao yaliyofungwa kati ya Oktoba 3, mwaka 2013 hadi Septemba 26.
    Mashabiki watapiga kura hadi Desemba 1 kwenye Tovuti ya FIFA ambako orodha ya wachezaji 10 itaopungua hadi kubaki watatu.
    Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka 2009, zikipewa heshima ya gwiji wa zamani wa Hungary na Real Madrid, Ferenc Puskas, imekwishachukuliwa na nyota kama Cristiano Ronaldo, Hamit Altintop, Neymar, Miroslav Stoch pamoja na Ibrahimovic miaka iliyopita.
    Ibrahimovic won the prize last year for his outstanding overhead kick for Sweden in their 4-2 friendly win against England
    Ibrahimovic alishinda tuzo hiyo mwaka jana baada ya bao aliloifungia Sweden kwa tik tak katika ushindi wa 4-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya England
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IBRAHIMOVIC APAMBANISHWA NA VAN PERSIE NA DIEGO COSTA TUZO YA BAO BORA LA MWAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top