UBELGIJI imeichapa mabao 3-1 Iceland katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa usiku wa kuamkia leo.
Ubelgiji walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Nicolas Lombaerts dakika ya 12 aliyemalizia mpira wa adhabu wa Adnan Januzaj, kabla ya Iceland kusawazisha kupitia kwa Alfred Finnbogason dakika ya 13.
Divock Origi aliyetokea benchi, akaifungia Ubelgiji bao la pili dakika ya 62, kabla ya Romelu Lukaku kuupamba kwa ushindi kwa bao la tatu dakika ya 73.
Kikosi cha Ubelgiji kilikuwa: Courtois, Vanden Borre, Alderweireld, Lombaerts, Vertonghen, Witsel, Dembele/Lukaku dk46, Fellaini, Januzaj/Mertens dk63, Hazard/Origi dk46 na Benteke/Praet dk76.
Iceland: Kristinsson/Jonsson dk46, Magnusson, Ragnar Sigurdsson/Eyjolfsson dk84, Jonasson, Saevarsson, Danielsson/Ari Freyr Skulason dk72, Gunnarsson/Birkir Bjarnason dk46, Gudmundsson, Gislason, Kjartansson/Bodvarsson dk74 na Finnbogason.
Kiungo wa Manchester United, Adnan Januzaj, kulia akiichezea Ubelgiji jana
Marouane Fellaini wa Ubelgiji kulia akipambana na Helgi Valur Danielsson wa Iceland
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2832147/Belgium-3-1-Iceland-Divock-Origi-shows-Liverpool-missing-Brussels-cracker.html#ixzz3IuiiAvkY
0 comments:
Post a Comment