• HABARI MPYA

    Sunday, November 09, 2014

    IVO MAPUNDA ANADAKA LEO SIMBA NA RUVU

    Kipa Ivo Mapunda atasimama langoni Simba SC ikimenyana na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivo aliumia mwishoni mwa Septemba na tangu hapo amekuwa nje akipata tiba. Katika kikosi cha leo, Ivo atacheza pamoja na William Lucian 'Gallas', Mohamed Hussein 'Tshabalala', Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano 'Messi', Awadh Juma, Amisi Tambwe, Said Ndemla na Emmanuel Okwi.
    Kwenye benchi wapo Peter Manyika, MIraj Adam, Joram Mgeveke, Perre Kwizera, Elias Maguri, Abdallah Seseme na Uhuru Suleiman.    

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVO MAPUNDA ANADAKA LEO SIMBA NA RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top