• HABARI MPYA

    Thursday, November 13, 2014

    MOYES APASUA JIPU BAADA YA KUPATA KAZI HISPANIA; "TIMU KIBAO ENGLAND ZILINITAKA"

    KOCHA David Moyes ametambulishwa rasmi kuanza kazi Real Sociedad katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini San Sebastian.
    Mwalimu huyo wa zamani wa Manchester United na Everton alizungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza tangu itangazwe atakuwa kcoha wa timu hiyo ya La Liga na akasema alipata ofa kibao za kuendelea kufundisha Ligi Kuu ya England.
    "Ili kujisikia kikamilifu kama kocha, inabidi ujaribu utamaduni tofauti. Wakati wote nilitaka kufanya kazi nje.
    David Moyes was unveiled to the press in San Sebastian on Thursday afternoon
    David Moyes akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa utambulishio wake leo mchana 
    Moyes (right) shakes hands with Director General Lorenzo Juarros prior to his first training session
    Moyes (kulia) akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu, Lorenzo Juarros kabla ya kuongoza mazoezi yake ya kwanza

    "Sikuwahi kuwa na shaka yoyote (kwamba nitarudi kwenye soka). Nilikuwa nia ofa kibao za kufundisha Ligi Kuu. Lakini hii ni nafasi ya kufundisha La Liga. Nafikiri imeipiku Ligi Kuu, kwa sababu ya ubora wa timu, kupata nafasi za kawaida kucheza Ligi ya Mabingwa,".
    Alipoulizwa ni timu ili ya Ligi Kuu England ilimtaka, Moyes alikataa kuzungumzia hilo, akisema; "Siwezi kufanya hivyo. Unajua hiyo si tabia yangu,".
    David Moyes amesaini Mkataba wa miezi 18 na Sociedad, na Mscotland huyo anajiunga na Real Sociedad ikiwa katika hali mbaya kwenye La Liga.  
    The Real Socidad squad gather in a circle as they meet their manager for the first time since his appointment
    Wachezaji wa Real Socidad wakiwa na kocha wao mpya kwa mara ya kwanza leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOYES APASUA JIPU BAADA YA KUPATA KAZI HISPANIA; "TIMU KIBAO ENGLAND ZILINITAKA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top