• HABARI MPYA

    Friday, November 14, 2014

    QATAR KUPEWA UENYEJI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2015

    KATIKA hali isiyotarajiwa, taifa tajiri la mafuta, Qatar inaweza kupewa uenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Januari, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Ufaransa. 
    Nchi nyingine za Afrika zinazoomba uenyeji wa michuano hiyo ni Nigeria, Gabon na Misri na katika nchi hizo tatu, moja itarithi nafasi ya Morocco iliyopokonywa uenyeji kwa kugoma kufanya Januari ikihofia ugonjwa wa Ebola unaoshambulia Magharibi mwa Afrika. 
    Iwapo Qatar itapewa uenyeji, hii itakuwa mara ya kwanza AFCON kufanyika nje ya Afrika, Mashariki ya Kati. 
    “Ikiwa Qatar itaombwa rasmi iko tayari kutoa msaada wowote kuandaa Kombe la Afrika katakana na uhusiano wake mzuri na Rais wa CAF, Issa Hayatou,” amesema Sheikh Hamad bin Khalifa bin Ahmed al-Thani, Mkuu wa Chama cha Soka Qatar.
    Na kwa Waqatari, itakuwa ni fursa nzuri kukuanya uzoefu kabla ya kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022. Pia itaipa fursa FIFA kuipima nchi hiyo kabla ya Kombe la Dunia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: QATAR KUPEWA UENYEJI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top