Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
FRIENDS Rangers imeendelea vyema na mbio zake za kuelekea Ligi Kuu, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Majimaji ya Songea jioni ya leo Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Rangers ya Manzese inafikisha pointi 19 na kupanda kileleni mwa Kundi A, wakiishushia nafasi ya pili Majimaji, ambayo inabaki na pointi zake 18.
Sifa zimuendee Almasi Mkinda aliyeifungia bao la ushindi Rangers ‘Wakombozi wa Manzese’ dakika ya 70 akimalizia kazi nzuri ya Yussuf Mgwao aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa tayari zimefungana bao 1-1, Rangers wakitangulia na Majimaji kusawazisha mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Eliteul Justin alitangulia kuifungia bao Rangers dakika ya tisa, kabla ya Marcel Boniventura kuisawazishia Majimaji dakika ya 45 kwa penalti, baada ya mshambuliaji Kudra Omary kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Wachezaji watatu wa zamani wa Yanga SC walikutana uwanjani leo, Kudra Omary, Freddy Mbuna walioichezea Majimaji na Cred Mwaipopo aliyeichezea Rangers.
Wachezaji wawili wa zamani walioanzia Simba B hadi kupandishwa kikosi cha kwanza, walikutana pia uwanjani leo, Marcel Boniventura aliyechezea Majimaji na beki Hassan Haitbu aliyechezea Rangers.
Kikosi cha Rangers kilikuwa; Alphonce Raphael, Twalib Athumani, Mtoo Hamisi, Hassan Hatibu, Samuel Mathayo, Almasi Mkinda, Khalid Twahir/Ambokile George dk83, Mussa John ‘Rooney’, Eliutel Justine/Karim Sule dk73, Credo Mwaipopo/Yussuf Mgwao dk82 na Iddi Ismail.
Majimaji FC; Oddo Nombo, Freddy Mbuna, Ally Mohamed, Sadiq Gawaza, Samir Said, Alex Zegega, Gerald Mbena/Mrisho Said dk64, Kudra Omary/Mohamed Omary dk76, Ditram Nchimbi, Marcel Boniventura na Frank Sekule/Oswald Issa dk60.

![]() |
Wachezaji wa Rangers wakishangilia ushindi wao leo |

Kiungo wa Rangers, Credo Mwaipopo aliyeruka juu kupiga kichwa dhidi ya mabeki wa Majimaji leo |
0 comments:
Post a Comment