• HABARI MPYA

    Monday, June 01, 2015

    AZAM FC YAMTENGEA 'KITITA' CHA MIAKA MIWLI AME ALLY WA MTIBWA SUAGR

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    AZAM FC inataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mkali wa mabao wa Mtibwa Sugar, Ame Ally (pichani kushoto).
    Ame anaweza kusaini Mkataba wa miaka miwili Azam FC, iwapo klabu hiyo itafikia makubaliano na Mtibwa Sugar, ambako amebakiza Mkataba wa mwaka mmoja.
    Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema; "Tupo kwenye mazungumzo na klabu yake, yule mchezaji bado ana Mkataba na Mtibwa, hatujamalizana,"amesema. 
    Ame ambaye msimu huu ametikisa nyavu za vigogo wote, Yanga, Simba na Azam ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na Mtibwa Sugar kiasi cha kuzivutia timu nyingi nchini.
    Imekuwa bahati yao Azam FC wameinasa saini ya mshambuliaji huyo mrefu mkali wa vichwa na mwenye mashuti makali.
    Akisajiliwa Ame, safu ya ushambuliaji ya Azam FC itasheheni kisawasawa, kwani tayari inao wakali kama Kipre Tchetche, John Bocco, Didier Kavumbangu na Gaudence Mwaikimba.
    Azam FC ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu nyuma ya Yanga SC waliobuka mabingwa.
    Mwakani, mabingwa hao wa zamani watacheza Kombe la Shirikisho la Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMTENGEA 'KITITA' CHA MIAKA MIWLI AME ALLY WA MTIBWA SUAGR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top