![]() |
Thomas Ulimwengu kushoto akitafuta maarifa ya kumtoka mchezaji wa Lupopo jana |
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa TPM, Ulimwengu aling’ara mno na kufunga mabao mawili mazuri, huku mengine yakifungwa na Cheibane Traore na Adama Traore.
Mabao hayo ya Ulimwengu ambaye Lubumbashi anaitwa Rambo, ni salamu kwa Misri ambayo itacheza na Tanzania katikati ya mwezi huu katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Lubumbashi leo, Uli ‘Rambo’ alisema; “Nimefurahi sana nimefunga mabao na kuisaidia timu yangu, lakini kikubwa nafurahi nipo katika kiwango kizuri kuelekea mechi yetu na Misri,”amesema.
0 comments:
Post a Comment