• HABARI MPYA

    Monday, June 01, 2015

    AMRI KIEMBA, MWAIKIMBA ‘WATUPIWA VIRAGO’ AZAM FC

    Amri Kiemba amecheza mechi 20,  tangu atue Azam FC Januari mwaka huu, nyingi akitokea benchui tena dakika za lala salama 
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Amri Ramadhani Kiemba na mshambuliaji Gaudence Exavery Mwaikimba ‘wametemwa’ Azam FC baada ya kumaliza mikataba yao.
    Taarifa ya Azam FC, ambayo pia imesema hadi sasa haijasajili mchezaji mpya, imeeleza kwamba mbali na wakongwe hao wawili waliowahi kucheza pamoja Yanga SC, kipa Jackson Wandwi pia ametemwa.
    Kiemba, aliyecheza mechi 20,  tangu atue Azam FC Januari mwaka huu, nyingi akitokea benchi tena dakika za lala salama, alikuwa Chamazi kwa mkopo kutoka Simba SC, ambayo ilimruhusu akamalizie Mkataba wake huko baada ya kuona ‘hana faida’ katika timu yao.  
    Mwaikimba alisajiliwa miaka minne iliyopita kutoka Prisons ya Mbeya, wakati Wandwi ni mlinda mlango aliyepandishwa kutoka akademi ya timu.
    Aidha, Azam FC pia imerefusha mikataba ya wachezaji wake tisa waliokuwa wakikaribia kumaliza mikataba yao. 
    Hao ni mabeki Said Mourad, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Brison Raphael, viungo Khamis Mcha ‘Vialli’, Joseph Kimwaga, Mudathir Yahya na Farid Mussa na mshambuliaji Dedier Kavumbagu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMRI KIEMBA, MWAIKIMBA ‘WATUPIWA VIRAGO’ AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top