Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
NILIKUWA Mdogo na kilichonistua ni hatua ya Mama Yangu `kuweweseka` huku na huko na aliacha kufua Nguo kisha kuanza kung’ang’ania Radio huku akilia.
Alikuja Rafiki Yake aitwae Mama Leila akamuuliza vipi`Mama Hussein mbona unalia? Mama Yangu akajibu huku akilia ``Jamani naskia Hemed Maneti amefariki Dunia``.
Hapo Ndipo Nilipobaini kuwa Hemed Maneti Ulaya Chiriku ameaga Dunia .
Ilikuwa ni Alhamisi miaka 25 iliyomalizika ,Ilikuwa Mei 31,1990 saa 11 jioni Katika Hospitali ya Mwananyamala Ulikuwa wakati wa Taifa la Tanzania kupata `Pigo` kwakuondokewa na `jabali la Muziki,Chiriku, kada wa umoja wa vijana wa ccm mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM.
Ni miaka Mingi Iakini ni wazi kuwa watu aina ya Hemed Maneti huwa hawafi ,wataendelea kuishi dahary na dahary pamoya na kuwa mwili wake upo ndani ya Kinywa cha Ardhi.
Utofauti wa Wanaojiita wanamuziki wa sasa nawa kipindi cha Maneti hauhitraji elimu ya kiwango cha juu sana kutambua hilo. Angalia tu `ujinga` wa baadhi ya wanamuziki wa sasa alafu tafuta historia ya kweli ya wanamuziki wa kipindi cha Maneti angalia uwezo wao ambao siyo copy ya magharibi.
Hemed alikuwa kiongozi na mwimbaji wa Vijana Orchestra kwa karibu miaka 16 aliacha pengo kubwa siyo kwa bendi yake tu, bali kwa taifa zima, ambalo bado lilikuwa likiuhitaji mchango wake kwa hali na mali na hata chama cha Mapinduzi .
Hemed alizaliwa katika kijiji cha Mamboleo, wilayani Muheza, Tanga mwaka 1954, alizikwa kijijini kwake baada ya umati mkubwa wa mashabiki na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake kutoa heshima zao za mwisho huku wengine wakiwa hawaamini kilichotokea.
Sauti ya Maneti isiyomithilika mpaka leo naisikiliza Radioni na katika kanda ama cd zake sijaona alofanana naye hata kidogo,Tungo za Maneti bado sijaona alofanana naye.
Kipaji cha utunzi na uimbaji alichojaliwa na KARIMA kilionekana wazi katika tunzi zake MURUWA Kuna msururu mrefu wa sifa na mchango mkubwa alioutoa marehemu Maneti katika mambo mbalimbali kupitia sanaa ya muziki.
Unaweza kusema kwamba, kwa vile bendi ya Vijana Orchestra ilikuwa, na bado, inamilikiwa na Umoja wa Vijana wa CCM, ndiyo sababu Maneti alikuwa akiimba nyimbo za siasa. Lakini ukweli unabaki wazi kwamba, mwanamuziki huyo alikuwa mwanasiasa safi ambaye hakuhutubia kwenye mikutano ya siasa, bali aliuonyesha uanasiasa wake kupitia jukwaa la muziki na mifano ipo mingi.
Maneti alitunga nyimbo nyingi za siasa na moja kati ya kazi zake bora ni ule wimbo wa Ally Hassan Mwinyi apewe kura za Ndiyo alioutunga mwaka 1985 katika kumpigia debe aliyekuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa wakati huo, Rais Mstaafu wa pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi.
Wimbo huo ulipigwa kila siku na Radio Tanzania na kutokea kupendwa sana na watu wakiwemo viongozi wa kisiasa, na ubora wa wimbo ulionekana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1990 pale bendi yake ya Vijana ilipoukarabati na kuutumia tena kwenye kampeni za Rais Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dakta Salmin Amour Juma.
Aidha, Maneti hakuwa nyuma katika masuala ya ukombozi pamoja na kutetea amani na alidhihirisha wazi kwamba ni mtetezi wa amani alipotunga wimbo safi wa Magaidi wa Msumbiji mwaka 1987. Wimbo huu pia ulitokea kuwa kipenzi cha watu na ni moja kati ya kazi za kukumbukwa.
Nyimbo nyingine za siasa ni Muungano umekamilika, Rushwa adui wa haki, Vijana nguzo na jeuri ya Chama, Operesheni Maduka, Mwenge umulike nje ya mipaka ya Tanzania, Tamasha la Vijana Moshi na nyinginezo nyingi.
Alijiunga na bendi ya Vijana Orchestra mwaka 1974 akitokea katika bendi ya TK Lumpopo iliyokuwa ikiongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini, Juma Kilaza, ambaye ni shemeji yake, na tangu alipoingia Vijana akapewa uongozi msaidizi wa bendi hadi mwaka 1982 alipoteuliwa kuwa kiongozi wa bendi.
Kuna Nyimbo Nyingi za Maneti ambazo ukisikiliza utabaini umahiri wake ambao haujafikiwa na yeyote mpaka sasa sikiliza Masimango, Mwanaume gani anasuka nywele, Nsabi, Kamata Ooh Sukuma, Matata Matata, Watoto wanalia sana, Mudinde acha fitina, Ooh Masido, Amba kawa baharia, Acha acha ngoma Jirekebisheni, Wifi zangu, Wajue wana Koka, Bujumbura na Safari yetu Zambia ambao haukurekodiwa.
Maneti hakuwa mwanamuziki wa kubahatisha wala kubabaika. Alikuwa ni mvumilivu na wala hakubweteka na umaarufu kwa muda wote aliokuwa na Vijana Orchestra.
Wanamuziki wengi walikuwa wakiingia bendi hiyo na kutoka, lakini kamwe Maneti hakutingishika licha ya vishawishi vingi kutoka bendi kadhaa za hapa nchini ambazo zilikuwa zikimtafuta kila kukicha ili aende katika Bendi zao.
Kutokana na uongozi wake imara bendi hiyo haikuyumba chini yake hata pale wanamuziki wake nyota walipokuwa wakihama. Baadhi ya wanamuziki ambao waliihama bendi hiyo katika vipindi tofauti na kusababisha mapengo makubwa katika bendi hiyo ni kama vile Cosmas Thobias Chidumule, George Mpupua, Hassan Dalali, Komandoo Hamza Kalala ambaye aliondoka na baadaye kurejea tena kabla ya kuihama tena na kwenda Washirika Tanzania Stars 'Watunjatanjata' pamoja na Eddy Sheggy na Adam Bakari 'Sauti ya Zege' waliokuwa nyota katika bendi hiyo.
Katika Mapenzi Maneti aliuvaa uhusika moja kwa moja ,sikiliza wimbo Stella,na jina Stella kwa maneti lina maana nyingi sana,yupo stela wa Kenya yupo Stella wa Tanzania wapo akina Stella Ndugu zake.
Chama cha Mapinduzi ccm kina dhamana kubwa kutunza na kumuenzi Hemed Maneti kutokana na Mchango mkubwa aliyoutoa kwa chama hicho na Taifa kwa ujumla.
Maneti huwezi kumuondoa na kina Bi. Shakila Said katika kulitetea Taifa la Tanzania kwakutumia sanaa ya uimbaji.
Msikilize bi Shakila katika wimbo `viva samora,viva msumbiji` msumbiji kukomboka sisi twaona fahari,leo twakuvika taji mpendwa Ndugu Somora.
Sisi waandishi wa Habari tuna dhima kubwa ya kuukumbusha Umma juu ya wanamuziki wetu waliyoweka alama Tanzania.
Pia tuna Dhima Kubwa kuwaalaani wanamuziki wengi wa sasa wanaovunja maadili na miiko yetu kwakutembea ama kuimba majukwaani wakiwa `watupu` na kutoa maneno yenye ukakasi yasiyovikwa Nguo.
Mpaka ninapoandika makala haya sioni anayefanana na Hemed Maneti hata kidogo. Pumzika kaka Yangu Hemed Maneti nasi tu Nyuma yako ila utaendelea kuishi dahary na dahary.
(Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV, ambaye anapatikana kwa namba +255 655 250157 na +255 752 250157)

![]() |
| Marehemu Hemed Maneti enzi za uhai wake akiimba katika jukwaa la Vijana Jazz |

.png)
0 comments:
Post a Comment