WENYEJI, Ihefu SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
Yanga ilitangulia kwa bao la kiungo wake Muivory Coast, Pacome Zouazoua dakika ya nne, kabla ya Ihefu kuzinduka kwa mabao ya Lenny Kissu dakika ya 40 na Charles Ilamfya dakika ya 67.
Kwa ushindi huo, Ihefu inafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya saba, wakati Yanga inabaki na pointi zake tisa nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi nne.
0 comments:
Post a Comment