• HABARI MPYA

    Thursday, May 17, 2012

    AVB, MARTINEZ MMOJAWAO KOCHA MPYA LIVERPOOL


    EPL-Wigan Athletic v West Bromwich Albion,Roberto Martinez
    Martinez
    KLABU ya Liverpool imemtaja kocha Roberto Martinez kuziba nafasi ya Kenny Dalglish aliyefukuzwa.
    Kampuni ya Fenway Sports Group (FSG) ya Marekani, Wamiliki wa Wekundu hao wa Anfield, wamewasiliana na kocha huyo wa Wigan, Martinez wiki iliyopita na vuanzo vinasema Msyanyola huyo ana nafasi kubwa kukalia kiti cha Dalglish aliyefukuzwa leo.
    Aprili, mwaka huu Martinez alikwishaamua ataondoka Wigan licha ya mmiliki wa klabu hiyo, Dave Whelan kukanusha kwamba hakuna ombi rasmi walilopokea, Liverpool sasa inatarajia kumtwaa kocha huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye pia anawaniwa na Aston Villa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AVB, MARTINEZ MMOJAWAO KOCHA MPYA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top