• HABARI MPYA

    Sunday, May 20, 2012

    DI MATTEO HAJAWAHI KUTOKEA KOCHA WA MUDA KAMA YEYE


    Di Matteo
    Roberto Di Matteo
    KOCHA wa muda wa Chelsea, Roberto di Matteo alipoingia kwenye chumba cha Mkutano na Wandishi wa Habari kwa mazungumzo ya baada ya mechi saa 7:15 usiku wa jana, alijivunia mafanikio makubwa zaidi kwa kocha yeyote wa muda kuwahi kupata daima. Machungu ya Chelsea daima kukosa Kombe la Ligi ya Mabingwa tayari yalikua yamefutwa kwa dawa nyepesi kutamka, Ushindi.
    Didier Drogba
    Didier Drogba
    Didier Drogba alipojipanga, bila pupa,wasiwasi wala hofu na kuupiga mpira ule kumpita goalkipa wa Bayern, Manuel Neuer, mwenye sifa ya kuzuia mikwaju ya peneti na kuthibitisha ushindi wa 4-3 kupitia matuta, miaka mingi ya kosa kosa iliwatoka wachezaji wote,wafanyakazi na viongozi wa Chelsea.
    Hili lilifuatiwa na Drogba kuvua shati lake na kulipeperusha juu ya kichwa chake kuonyesha furaha ya ushindi baada ya kukimbia kuzunguka uwanja mzima, huku Fernando Torres na David Luiz wakipanda juu ya besera la goli kuonyesha furaha yao. Wakati huo Mmiliki wa klabu hio Abramovich mwenyewe akiruka na kupiga makofi huku akiimba ikidhihirisha sura isiyoonekana kwa kawaida kwa mtu msiri asiyeonyesha hisia zake.
    Ikiwa mkwaju huo ulikua wa mwisho kwa mchezaji huyu kutoka Ivory Coast kama mchezaji wa Chelsea, pamoja na bao lake la kusawazisha lile la Thomas Mueller, basi Drogba ataondoka kwa kuandikisha rekodi yake binafsi.
    Drogba mwenyewe hakuweza kuelezea bayana juu ya majaliwa yake baada ya kukabidhiwa zawadi ya mchezaji bora wa mechi hio ya fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya. Punde mkataba wake unafikia mwisho na bado hakuna matumaini ya kama ataongezewa mda.
    Hatma ya Meneja wa mda Di Matteo bado haijabainika na mwenyewe alishindwa kusema ni nini alidokezewa na Abramovich walipokumbatiana kwenye ngazi kabla ya sherehe za kukabidhiwa Kombe kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 107 ya klabu hio.
    Abramovich
    Abramovich
    Haikua kazi rahisi kwa Chelsea uwanjani mpira ulipochezwa katika sehemu ya uwanja ya Chelsea lakini hadi mwisho lakini waliepuka uwezekano mkubwa wa kufungwa zaidi ya mabao manne ila kutimiza ndoto ya Abramovich.
    Mara pekee kwa klabu hii kushamiri katika mashindano ya Ulaya, ulikua mwaka 1971 kabla ya hata Liverpool kushinda nje ya England, Chelsea ilipoichapa Real Madrid na kujishindia Kombe la Mshindi la mwaka huo wa 1971.
    Drogba, aliongoza na kua kinara, na hivyo kuandika jina lake kwa vitendo katika historia. Kipa Petr Cech amepitia kipindi kigumu wakati wa kampeni ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya lakini mjini Munich alionyesha ukomavu kwa kuzuia mkwaju wa Arjen Robben katika kipindi cha ziada na wakati wa matuta alizuia mkwaju wa Ivica Olic.
    Andre Villas Boas na Di Matteo
    Andre Villas Boas na Di Matteo
    Mwamko wa Chelsea ulianza pale alipotimuliwa Andre Villas Boaskufuatia kipigo cha 3-1 na Napoli na mrithi wake Di Matteoakageuka kua chachu ya ufanisi kwa kusababisha ushindi wa Kombe la FA na mechi kadhaa za Ligi kuu ya Premiership.
    Matokeo ya Napoli yakageuka kuipendelea Chelsea na baada ya hapo kuichabanga Benfica kujishindia fursa ya kukutana na Barcelona ambayo waliweza kuishinda kwa hatua zote mbili,nyumbani na ugenini licha ya kusukumwa kwa dakika nyingi.
    Sifa kubwa anastahili Roberto Di Matteo aliyechimba ndani ya bongo za wachezaji aliyewafahamu na kuamini kua wana uwezo wa kushiriki na kucheza soka kwa kiwango cha juu na kushinda.
    Bila shaka wadadisi watakosoa mbinu zilizotumiwa dhidi ya Barcelona na huko Munich lakini jibu la Di Matteo ni moja tu angalia rekodi ya mwaka 2012, Mabingwa wa Ulaya ni Chelsea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MATTEO HAJAWAHI KUTOKEA KOCHA WA MUDA KAMA YEYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top