• HABARI MPYA

    Tuesday, May 22, 2012

    DI MATTEO KUPEWA MWAKA MMOJA WA MAJARIBIO CHELSEA


    Roberto Di Matteo
    Getty Images
    MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich anajindaa kumpa mkataba wa mwaka mmoja wa majaribio, Roberto Di Matteo baada ya kuwa hajashawishika kiasi cha kutosha kumpa wadhifa kamili wa ukocha Mtaliano huyo, kwa mujibu wa gazeti la The Times.
    Tangu ateuliwe kama kocha wa Muda, kufuatia kufukuzwa kwa Andre Villas-Boas, Machi, mwaka huu, kocha huyo wa zamani wa West Brom amefanya makubwa Blues, akiiongoza kutwaa Makombe ya FA na Ligi ya Mabingwa.
    Na, wakati Abramovich hamchukulii Di Matteo kama kocha babu kubwa, ameafiki kwamba kijana huyo wa umri wa miaka 41 anastahili nafasi zaidi Stamford Bridge baada ya mafanikio ya msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MATTEO KUPEWA MWAKA MMOJA WA MAJARIBIO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top