• HABARI MPYA

    Tuesday, May 22, 2012

    OWEN MWINGINE NAYE ATUPIWA VIRAGO MANCHESTER


    Carling Cup: Owen Hargreaves, Manchester City v Birmingham
    Owen
    KIUNGO Owen Hargreaves ametemwa na klabu ya Manchester City, baada ya msimu mmoja wa kuwa na klabu hiyo.
    Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England alitua Etihad msimu uliopita, baada ya kumaliza mkataba Manchester United.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amecheza mechi nne tu kwa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu England msimu huu, akifunga bao moja tu katika mechi ya nyumbani na Birmingham City kwenye Kombe la Ligi, kwa shuti kali la umbali wa mita 20.
    Amekuwa akisumbuliwa na majeruhi msimu wote na klabu hiyo imethibitisha katika tovuti yake leo kwamba kiungo huyo wa zamani wa Bayern Munich ataruhusiwa kuondoka msimu huu.
    Hargreaves amekuwa akisumbuliwa na maumivu kwa misimu michache iliyopita, tangu akiwa Manchester United ingawa ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa na klabu hiyo msimu wa 2007/08.
    Mzaliwa huyo wa Canada, alilazimika kumuona mtaalamu wa goti Amerika mapema mwaka 2010 katika jitihada za kutatua tatizo lake sugu.
    Kufuatia kufanyiwa upasuaji, Hargreaves alicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu baada ya takriban miaka miwili dhidi ya Sunderland, lakini majeruhi zaidi yaliibuka.
    Alicheza mechi moja zaidi akiwa na jezi ya Mashetani Wekundu katika Kombe la Ligi dhidi ya Wolves Uwanja wa Old Trafford, Novemba mwaka huo, lakini akalazimika kutoka nje baada ya dakika 10 za mwanzoni, kufuatia maumivu ya nyama za paja.
    Kiungo huyo, ambaye ameichezea timu ya taifa ya England mechi 42, alihamia City msimu uliopita baada ya kutemwa na Sir Alex Ferguson, ili akaribu bahati yake sehemu nyingine, lakini ameshindwa pia kusimama imara na huko pia na anatemwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OWEN MWINGINE NAYE ATUPIWA VIRAGO MANCHESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top