• HABARI MPYA

    Wednesday, June 20, 2012

    20 BORA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012, HAKUNA MUINGEREZA, MFARANSA MMOJA TU

    Andrés Iniesta - Spain
    Iniesta
    Getty Images

    MABINGWA watetezi, Hispania wameongoza kundi lao, licha ya kupitia wakati mgumu, wakati washindi wa pili wa Euro 2008, Ujerumani wamemaliza hatua ya makundi kwa rekodi baab kuibwa kwenye Kundi la Kifo na Jamhuri ya Czech licha ya mwanzo mbaya wamefuzu pia na England wamewastaajabisha wengi kwa kuongoza Kundi D mbele ya Ufaransa ambao wamekuwa katika kiwango kizuri kabla ya michuano hii.

    Sasa mambo yameiva na kuelekea Robo Fainali, BIN ZUBEIRY kwa msaada wa Goal. com wanakuletea 20 Bora ya wachezaji waliofanya vizuri katika hatua ya makundi angalau kwa asilimia 40.

    WACHEZAJI  20 BORA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012
    NAMBAMCHEZAJIWASTANI WA KIWANGO
    1
    Andres Iniesta  ANDRES INIESTAUkraine
       
    2
      BASTIAN SCHWEINSTEIGER
       
    3
      MICHAEL KROHN-DEHLI
      
    4
      PEPE
      
    5
      NICKLAS BENDTNER
      
    6
      MATS HUMMELS
      
    7
      ANDREA PIRLO
      
    8
      ANDRIY SHEVCHENKO
      
    9
      XAVI
      
    10
      ZLATAN IBRAHIMOVIC
      
    11
      PHILIPP LAHM
      
    12
      MARIO GOMEZ
      
    13
      CESC FABREGAS
      
    14
      FRANCK RIBERY
      
    15
      JOAO MOUTINHO
      
    16
      DAVID SILVA
      
    17
      STEPHAN ANDERSEN
      
    18
      LUKA MODRIC
      
    19
      MESUT OZIL
      
    20
      SAMI KHEDIRA
      

    Katika orodha hiyo, Ujerumani imeingiza wachezaji sita wakati Hispania ina wanne. Andres Iniesta analingana na Bastian Schweinsteiger kileleni baada ya wote kufanya 'mavituuz' yanayoelekea kulingana katika hatua ya makundi.

    Denmark ina wachezaji wawili katika tano bora licha ya kutolewa, baada ya kufungwa na Ureno na Ujerumani.

    Pepe na Mats Hummels wamekuwa wagumu katika safu ya ulinzi wakati kiungo Xavi na Andrea Pirlo wametawala kwenye idara yao.

    Andriy Shevchenko na Zlatan Ibrahimovic wamo ndani ya 10 Bora ingawa makali yao hayakuzisaidia timu zao kuingia Nane Bora.

    Franck Ribery ni Mfaransa pekee ndani ya 20 Bora hiyo, wakati hakuna mchezaji hata mmoja wa England, licha ya Three Lions kuongoza kundi.

    Mario Gomez, ambaye anaongoza kwa mabao kwenye michuano hiyo hadi sasa, akiwa amefunga mara tatu, anashika nafasi ya 12 na Luka Modric ni mchezaji pekee wa Croatia katika orodha hiyo.

    Nyota wa Denmark, Stephan Andersen ni kipa pekee kwenye orodha hiyo, wakati viungo 13 wameingia kwenye orodha hiyo.

    Goal.com imekuwa ikifanya tathmini ya viwango vya wachezaji katika kila mechi kwenye hatua ya makundi na imeahidi kuendelea hadi mwisho wa michuano hii Julai 1, mwaka huu na BIN ZUBEIRY itaendelea kumulika huko, ili kuwaletea uhondo wasomaji wake.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 20 BORA HATUA YA MAKUNDI EURO 2012, HAKUNA MUINGEREZA, MFARANSA MMOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top