Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya
ROONEY UINGEREZA NZIMA
USHINDI wa England dhidi ya wenyeji Ukraine umeifanya Three Lions ikutane na Italia katika Robo Fainali, huku bao pekee la Wayne Rooney likatwala vichwa vya habari Uingereza.
The Sun limsema: Weave Done It - Roo heads winner with new hairdo
Daily Mail: Thatch the way to do it. Weave got Italy next, thanks to Rooney (and a useless official).
Daily Star: Hairoo - Wayne's gel of a guy to set up Italian job.
Daily Mirror: Too good to be Roo.
Independent: England get over the line.
The Times quotes Rooney saying: "We can end hoodoo."
INIESTA AAMINI HISPANIA HII NI KALI KULIKO YA KOMBE YA 2010
KIUNGO Andres Iniesta, mwenye umri wa miaka 28, anaamini kikosi cha sasa Hispania ni bora zaidi kile kilichotwaa Kombe la Dunia 2010 na kinaweza pia kuchukua ubingwa wa Euro 2012.
KOCHA wa Ukraine, Oleg Blokhin aliwakasirikia Waandishi baada ya kipigo cha England katika Euro 2012 baada ya kutaka mahojiano naye.
KOCHA wa Ujerumani, Joachim Loew amepuuzia yote yanayozungumzwa kuhusu timu yake na ubingwa wa Euro 2012.
BEKI wa Italia, Giorgio Chiellini, mwenye umri wa miaka 27, yuko shakani kucheza mechi ya Robo Fainali ya Euro 2012 dhidi ya England kutokana na maumivu ya nyama za paka.
AC MILAN WAMTAKA REINA
KLABU ya AC Milan inataka kumsajili kipa wa Liverpool, Pepe Reina, raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 29. Habari kamili: Daily Mail
KLABU ya Barcelona inasaka beki mpya na inawafikiria beki wa Arsenal, Thomas Vermaelen, mwenye umri wa miaka 26, beki wa Manchester City, Vincent Kompany, mwenye umri wa miaka 26 pia, na beki wa Chelsea, David Luiz, mwenye umri wa miaka 25, iwapo watamkosa beki wa Athletic Bilbao, Javi Martinez, mwenye umri wa miaka 23, ambaye ndiye chaguo lao la kwanza.
KIUNGO WA Manchester City, Nigel De Jong, mwenye umri wa miaka 27, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wake licha ya dalili kwamba anaweza kubaki na mabingwa hao wa Ligi Kuu.
OFISA Mtendaji Mkuu wa AC Milan, Adriano Galliani ameghairi mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na Italia, Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 21 aliyewahi kuchezea Inter Milan.
KLABU ya Sunderland imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji Louis Saha, mwenye umri wa miaka 33, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Tottenham, ikizipiku timu za Mashariki ya Kati.
KLABU ya West Ham imepandisha dau lake katika kuwania saini ya Grant Holt, mwenye umri wa miaka 31, hadi pauni Milioni 5.5, baada ya ofa yao ya awali ya pauni Milioni 3, kupigwa chini na Norwich.
KLABU ya Newcastle iko tayari kumsajili mshambuliaji wa FC Twente, Luuk de Jong, mwenye umri wa miaka 21, kwa kutoa dau la pauni Milioni 9, lakini imekwama kumsajili beki wa kulia wa Ufaransa, Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Lille.
MCHEZAJI Clint Hill, mwenye umri wa miaka 33, amesaini mkataba wa mwaka mmoja QPR - na kuzima ndoto za Leeds waliokuwa wanamtaka.
SPURS WATETA NA AVB
KLABU ya Tottenham imefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas na wako tayari kumpa ofa ya kurithi mikoba ya Harry Redknapp, aliyefukuzwa.
WAMILIKI wa klabu ya Watford, Wataliano wamemlenga mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Gianfranco Zola awe kocha mpya wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment