Ukraine imeibuka na ushindi wa 2-1 katika mchezo wao wa
kwanza Euro 2012, Kundi D dhidi ya Sweden, kwenye Uwanja wa NSK Olimpijs'kyj,
mjini Kyiv. Sweden walitangulia kupata bao kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic
dakika ya 52, akiunganisha pasi ya K. Kallstrom, kabla ya Andrey Shevchenko kuwasawazishia
Ukraine, wenyeji wa fainali hizo kwa pamoja na Poland dakika ya 55, akiunganisha
pasi ya A. Yarmolenko na baadaye Shevchenko akafunga la pili dakika ya 61, pasi
ya Y. Konoplyanka. Katika mechi ya awali ya Kundi D, kati ya England na
Ufaransa, timu hizo zilitoka sare ya 1-1. Pichani ni Shevchenko akifunga.
|
0 comments:
Post a Comment