![]() |
Kocha wa Serengeti Bosy, Jacob Michelsen (katikati) akiwa na mpenzi wake kushoto na kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen kulia. |
Na Prince Akbar
HABARI njema
kwa Watanzania. Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti
Boys imefuzu kucheza raundi ya Tatu na ya mwisho katika michuano ya kutafuta
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana wa umri huo, baada ya Misri
kujitoa.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, Serengeti Boys ilikuwa icheze Raundi ya pili
dhidi ya Misri; mchezo wa kwanza ukichezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es
Salaam na ule wa marudiano wiki mbili baadaye jijini Cairo, lakini wapinzani
wao wamejitoa.
Ikumbukwe, katika
raundi ya kwanza pia, Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka
Denmark ilipita bila jasho baada ya Kenya kujitoa mwezi uliopita na sasa njia
inazidi kuwa nyeupe kwa timu hiyo kukata tiketi ya kucheza Fainali za U17 za
Vijana zitakazopigwa mwakani nchini Morocco.
Wambura
alisema kwa matokeo hayo, sasa Serengeti Boys itacheza Raundi ya Tatu dhidi ya
mshindi wa mechi kati ya Zimbabwe na Kongo Brazzaville, mechi ya kwanza ikichezwa
Novemba 18 mwaka huu mjini Dar es Salaam na marudiano wiki mbili baadaye
ugenini.
Zimbabwe na
Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu,
Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano itafanyika kati
ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment